![](http://1.bp.blogspot.com/-LJkFASyqeDw/UcQII4mV2yI/AAAAAAAAh7Y/0TA5pWn0kUU/s1600/1.jpg)
HAUSIGELI ambaye jina lake halikupatikana mara moja, nusura ajirushe chini kutoka ghorofa ya pili kwa kile kilichodaiwa kuwa aliogopa moto mkubwa uliozuka katika jengo la jirani na ghorofa alilokuwemo. Tukio hilo lilijiri mapema asubuhi ya Juni 18, mwaka huu kwenye makutano ya Mtaa wa Nyamwezi na Mkunguni eneo la Kariakoo jijini Dar es Salaam. Kwa mujibu wa majirani, baada ya kuona moto huo ulioambatana na wingu zito la moshi ukitoka kwenye jengo la jirani, hausigeli huyo alitoka dirishani na kutaka kujirusha chini bila kujali nguo zilizokuwa zikimvuka katika purukushani hiyo. Alifanikiwa kukaa kwenye sehemu ya ukingo wa ghorofa...
SAKATA ZIMA LA KUPIGWA KWA MBUNGE WA KASULU ( MOSES MACHALI) AKIWA DODOMA JANA JIONI
![](http://2.bp.blogspot.com/-CjTFdGVXEs4/UcP69vtHVhI/AAAAAAAAh6w/xOKO1CBYBXo/s1600/MOSES.jpg)
Habari kutoka Dodoma zinasema Mbunge wa Kasulu Mjini kupitia chama cha NCCR-Mageuzi, Mhe. Moses Machali (pichani), amelazwa katika hospitali ya mkoa ya Dodoma kuuguza majeraha aliyoyapata baada ya kushambuliwa na watu wasiojulikana jana jioni mjini Dodoma. Tukio hilo lilitokea jana jioni wakati Mh. Machalli akiendesha gari lake mita kadhaa kutoka ilipo nyumba anayoishi baada ya kuwapigia honi vijana kadhaa waliokuwa wakitembea katikati ya barabara ili wasogee pembeni naye aweze kupita .... Kitendo hicho kilionekana kuwaudhi na kuwakera vijana hao ambao walianza kuipiga na kuigonga kwa nguvu bodi ya gari...
MABONDIA WANNE WA TANZANIA WAFUNGWA JELA MIAKA 15 BAADA YA KUNASWA NA MADAWA YA KULEVYA NCHINI MAURITIUS
![swacotz forum www.kassimngumbi.blogspot.com](http://2.bp.blogspot.com/-YTHaV4w-foo/UcP2MtjAnsI/AAAAAAAAh6g/_B-wfsOwx2M/s1600/2.jpg)
Mabondia wanne wa Tanzania wafungwa miaka 15 jela nchini Mauritius kwa makosa ya kuingiza dawa za kulevya aina ya heroin. Mabondia hao ni Case Ramadhani Fills, Nathanael Elia Charles, Ally Rajabu Msengwa na Petro Charles Mtagwa.Wakati kesi hiyo ilipoanza kusikilizwa, wote walikiri makosa ya kuingiza mihadarati hiyo nchini Mauritius wakati walipokwenda kushiriki mashindano ya ndondi barani Afrika mwaka 2008.Wakiwa mbele ya Jaji, waliiambia mahakama kuwa walilazimika kuingia katika biashara hiyo haramu kutokana na hali zao za maisha kuwa maskini. "Tunaomba radhi kwa taifa la Mauritius", waliiambia mahakama. "Tu watu maskini na...
MWANAFUNZI APIGWA RISASI TUMBONI CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM USIKU WA KUAMKIA LEO
![](http://3.bp.blogspot.com/-FM7iVAzFw04/UcPyXM3ikVI/AAAAAAAAh6Q/jaZ6hiu6GGk/s1600/1.jpg)
Taarifa zilizotufikia zinaeleza kuwa wanafunzi wanne wa chuo kikuu cha Dar es salaam wamevamiwa na majambazi usiku wa kuamkia leo maeneo ya Yombo chuoni hapo. Wanafunzi hao wanaosemekana kuwa ni wa mwaka wa nne na wa mwisho wa masomo walikuwa wanajisomea na kuandaa “Disertation” zao na kujikuta wakivamiwa na watu wanne na kuamuriwa watoe kompyuta zao na pochi za fedha. Kwa mujibu wa chanzo cha habari hii kutoka chuoni hapo, wanafunzi hao walikubali kuwapa kompyuta hizo na pochi za fedha, na majambazi kuanza safari yao ya kuondoka bila kuwadhuru.Baadaye wanafunzi hao wakawaomba wapate hata
No comments:
Post a Comment