Utabiri wa wengi kuwa ushosti wa waigizaji masistaduu wa Bongo Movies, Wema Isaac Sepetu na Kajala Masanja kutumbukia nyongo unadaiwa kutimia na sasa wametibuana, Habari za ndani kutoka kwa mtu wa karibu (jina linahifadhiwa), mwanzoni baada ya Wema kumlipia Kajala faini ya Sh. milioni 13 na kumnusuru kutokwenda Segerea a.k.a Segedansi, wawili hao walikuwa marafiki kama pete na kidole. “Walishinda wote, walilala wote, walikwenda klabu wote yaani Kajala alikuwa anamnyenyekea ‘madam’ Wema kwa kumuepusha na kifungo cha miaka 7 jela,” kilisema chanzo chetu na kuongeza: “Kuna wakati hapa katikati Kajala alikuwa kama...
"SIKU YA MAZISHI YANGU WATAJAA WATOTO NA MASHOGA TU"....AUNT LULU
![](http://3.bp.blogspot.com/-yVKQW6SF2kg/UcQPtm6jvwI/AAAAAAAAh74/c7IYmVyAVo8/s1600/3.jpg)
MSANII wa filamu Bongo, Lulu Mathias ‘Aunty Lulu’ amefunguka kuwa siku akifa anaamini mbali na watu wengine mazishi yake yatatawaliwa na mashoga pamoja na watoto. Akizungumza na mwandishi wetu hivi karibuni, Aunty Lulu alisema kutokana na ukweli kwamba wengi wanaompenda na ambao wamemzoea ni watoto waliokuwa wakimsikiliza kwenye Kipindi cha Watoto Shoo kupitia Radio One na ITV na mashoga ambao awali alikuwa kama mama yao, hao ndiyo watakaojaa kwenye mazishi yake. Alisema sababu kubwa ya msiba wake kujaa mashoga wengi ni kwa kuwa kabla hajabadili mfumo wa maisha anayoishi sasa, alikuwa akiwalea hivyo siku ya mazishi...
MAKAMPUNI YA SIMU YATAPANDISHA GHARAMA ZA MAWASILIANO IFIKAPO TAREHE MOJA MWEZI WA SABA
![](http://1.bp.blogspot.com/-JE6BbloY4fE/UcQM3sSYqwI/AAAAAAAAh7o/vT0ay_Yb7_c/s1600/MOATI.jpg)
Kufuatia kuongezwa kwa kodi katika huduma za simu za mkononi , gharama za huduma hizo zinatajiwa pia kuongezeka kuanzia Julai Mosi mwaka huu. Taarifa ya pamoja iliyotolewa jijini Dar es salaam na Umoja wa Makampuni ya Simu za Mkononi Tanzania – MOAT imesema pendekezo la serikali la kuweka kodi ya 14.5 kwenye huduma za simu za mkononi hazotoweza kukwepesha kupanda kwa gharama za simu kwa watumiaji. MOAT inasema awali kodi ilikuwa ikitozwa asilimia 12.5 katika huduma ya mawasiliano ya simu na kwmaba ongezeko la kufiikia asilimia 14.5 tofauti na nchi za jirani Kenya na Uganda ambazo zimeendelea kutoza viwango vya ushuru vya asilimia...
No comments:
Post a Comment