EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Friday, June 21, 2013

PETER CHAMI: DAMU HAIUZWI HOSPITALINI NA ANAYEFANYA HIVYO NI MWIZI NA AWAJIBISHWE KAMA MLA RUSHWA

Wizara ya afya na ustawi wa jamii nchini katika kuhakikisha inakuwa na akiba ya damu ya kutosha kwa ajili ya wananchi wake bado inaendelea na utaratibu wa mpango wa damu salama kwa kukusanya damu tka kwa wananchi kote nchini na kuzihifadhi kwa matumizi ya watu mbalimbali 
Peter Chami-mkuu wa timu ya damu salama dar es salaam
akielezea suala hilo mkuu wa kikundi cha ukusanyaji damu kutoka ofisi ya damu salama kanda ya mashariki ambayo inahudumia mikoa ya MOROGORO,DAR ES SALAAM NA DODOMA bw:Peter Chami alisema wananchi wanatakiwa kujua umuhimu wa kujitolea damu kwakuwa zinawasaidia wao na ndugu zao pindi wanapougua hivyo alishauri wawe wanajiwekea tabia ya kufanya hivyo kwani ni kindendo ambacho ni cha kiuungwana hata hivyo
wahudumu wa kikundi wakimhudumia mchangia damu
 bw:Chami alikanusha kuwa hairuhusiwi kwa mtu yeyote kununua damu anapofika hospitalini na wao kama wizara wanalisimamia hilo ingawa bado kuna watu ambao sio waaminifu wanajaribu kuwalaghai wananchi kwa kuwatoza pesa kwa ajili ya kuwekewa damu,katika hilo mkuu huyo alisema kuwa wizara inatoa damu katika hospitali zote zikiwemo zile za watu binafsi.
wahudumu wa kikundi wakimhudumia mchangia damu
Bw:Chami alisema hayo alipozungumza na Swacotz Katika viwanja vya chuo cha uandishi wa habari Royal jijini Dar es salaam wakati akisimamia  zoezi la utoaji damu lakini kiongozi huyo aliwataka watu wanaotoa damu kuzingatia vigezo na kanuni za utoaji damu kama vile kuwa na umri zaidi ya miaka 18,uzito usiopungua kg50,usiwe katika wakati wa dozi au siku zako kwa wasichana au wanawake,msafara huo ulikuwa ni pamoja na wasaidizi wake Ene Grace Nkya,Haidani ndimbo,na Linus Kapuya na inasadikika kuwa mtu mwenye uzito wa kg50 anauwezo wa kutoa damu zaidi ya Mililita 5000 mpaka 7000 sawa na lita 5000 mpaka 7000.



www.kassimngumbi.blogspot.com
Add caption
ENEO LA MAALUM LILILOTUMIKA KWA SHUGHULI YA KUCHANGIA DAMU  RCT

No comments:

Post a Comment