NA
MSHAMU NGOJWIKE
Hafla
hiyo ya kupima afya jana asubuhi,ilifanyika kwenye Hospitali ya Wilaya ya
Kinondoni ya ‘Mwanyamala’ ikiongozwa na viongozi wa Klabu pamoja na benchi la
ufundi.
Akizungumza
na SWACOTZ FORUM jana, Katibu Msaidizi wa Ndanda Fc, Selemani Kachele alisema
wamefikia hatua hiyo ya kuwatambua hali zao za kiafya wachezaji wote kabla ya
kuanza msimu wa Ligi Kuu Tanzania Bara(VPL).
“Tunapima
afya zetu kwa ujumla ili kubaini matatizo ya kiafya wachezaji tuliowasajili
kabla ya kuanza kwa Ligi msimu huu, uwezi kuingia kwenye vita bila kukagua
silaha zako kama zina mtatizo au laa!, tunataka kutambua ufitness wao,isije
mchezaji michezo miwili mitatu yupo benchi kwa maumivu,”alisema.
Aliesma
taratibu hii ya kupima afya ya wachezaji itakuwa endelevu ya kubaini matatizo
yao ya Kimwili kabla ya kushiriki mashindano ya aina yeyote hapa nchini.
Ndanda
Fc,ipo kwenye maandalizi ya msimu wa
Ligi kuu Tanzania Bara inayotarajia kuanza kunguruma Septemba 20 mwaka huu, kwa
kuweka kambi ya siku 40, katika Chuo Kikuu cha Ardhi jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment