EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Thursday, August 7, 2014

KARIM BENZEMA SASA 'KUZEEKEA' REAL MADRID



MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Ufaransa, Karim Benzema ameongeza mkataba wa kuendelea kuichezea Real Madrid ya huko nchini Hispania mkataba ambao utambakisha klabuni hapo hadi mwaka 2019.

Benzema amesaini mkataba huo mara  baada ya kukataa kuhamia kunako timu za Ligi Kuu nchini uingereza ambako alihusishwa na taarifa za kuhitajika na vilabu mbalimbali vya nchi hiyo.

Hivi karibuni Kulikuwa kuna tetesi kwamba mpachika mabao huyo wa Ufaransa anaweza kuondoka klabu hiyo ya Hispania, lakini sasa wazi ataishi Bernabeu hadim mwaka 2019.

Hivyo kuviacha midomo wazi vilabu vya Arsenal, Liverpool na Tottenham Hotspur vyote kutokea uingereza ambavyo ni miongoni mwa timu za Ligi Kuu nchini humo zilizokuwa zinamtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26.

No comments:

Post a Comment