NA: KASSIM NGUMBI
Mkuu wa wilaya ya mtwarai MH: Williman Kapenjama Ndile
amezipongeza shule zilizofanya vizuri toka manispaa ya mtwara mikindani katika
matokeo ya mitihani ya mwisho kwa upande wa shule za msingi na sekondari iliyofanyika kitaifa mwishoni mwa mwaka 2013
huku akiziasa shule ambazo hazikufanya vizuri kwa mwaka huu kujipanga na
kuchukulia hiyo kama sehemu ya changamoto kwao ili kufaulisha wanafunzi wao
vizuri hali itakayoplekea kupanda kwa kiwango cha elimu na kufikia lengo la
serikali la matokeo makubwa sasa.
Akizungumza katika sherehe za wiki ya elimu kiwilaya kwa
ngazi ya wilaya zilizofanyika leo katiuka vuwanja vya mashujaa mtwara mikindani
MH: Ndile ambaye pia alikuwa ninmgeni rasmi alisema kuwa mtwara ilizamiria
kufanya vizuri katika elimu kwa msimu uliomalizika na inayoendelea na hicho
ndicho kilivhofanyika na kueleza kuwa ni
fahari kubwa kuona shule nyingi zimeweza kufanya vizuri kuanzia zile binafsi
mpaka za serikali.
Awali wakati akitoa shukrani zake aliwataka walimu wa shule
zilizofanya vizuri kutojisahau kwa matokeo waliyoyapata badala yake waongeze
bidii ili kufika mbali zaidi lakini pia alizitaka shule zilizofanya vibaya
kuhakikisha zinafuta matokeo hayo katika mitihani ijayo na kwenda na kasi
itakayowapelekea kwenda sambamba na juhudi za serikali za kukuza elimu nchini
inayotambulika kama matokeo makubwa sasa.
Katika ghafla hiyo mkuu wa wilaya alikabidhi zawadi kwa shule
zipatazo 13 zilizofanya vizuri na zile zilizofanya vibaya za msingi na
sekondari ambapo kwa upand wa shule za msingi zilizofanya vizuri ni king david,
rahaleo, na kambarage na zilizofanya vibaya ni LWELU, MITENGO, na likonde
wakati za sekondari zilizofanya vizuri ni AQUINAS, MTWARA UFUNDI na SHANGANI na
zilizofanya vibaya ni MANGAMBA huku shule zilizoboreka kitaaluma zikiwa mbili
nazo ni shule ya sekondari CHUNO na shule ya sekondari ya NALIENDELE.
No comments:
Post a Comment