EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Tuesday, April 1, 2014

VURUGU ZA BUNGENI WATATU WAKAMATWA WAKIDAI HATI YA MUUNGANO KWA KAMATI ZA BUNGE

 
Mwenyekiti wa Kamati namba tatu ya Bunge Maalumu la Katiba, Shamsi Vuai Nahodha  akiongoza mjadala wa kikao cha kamati hiyo mjini Dodoma jana. Kulia ni mjumbe wa kamati hiyo, Anne Makinda. Picha na BMK 

Dodoma. Bunge la Katiba jana lilianza kujadili Rasimu ya Katiba kwa misukosuko kwenye Kamati baada ya kuvamiwa na kundi la wanaharakati waliokuwa na mabango wakidai hati halisi ya Muungano yenye saini za Mwalimu Julius Nyerere na Abeid Karume.
Msukosuko mwingine uliozikumba karibu kamati zote zinazoanza kujadili rasimu hiyo kwa kuanzia sura mbili zinazohusu Muungano – sura ya kwanza na ya sita na kuzua malumbano, ni maana ya maneno dola, shirikisho, muungano na nchi.
Wakati waandamanaji wenye mabango wakiishia mikononi mwa polisi, suala la Muungano lilitulizwa kwa kuitwa wanasheria kutoa tafsiri sahihi kwa kila neno.
Katika kamati zote, suala la muda wa kamati kujadili sura hizo mbili kwa siku mbili kila moja pia liliibua mjadala mkali, hadi kuwalazimisha baadhi ya wenyeviti wa kamati kuamua kumwandikia mwenyekiti wa Bunge, Samuel Sitta kuomba muda uongezwe.
Hali hiyo imejitokeza Bunge hilo likiwa limeshakaa siku 40 kabla ya kuingia katika mjadala rasmi, baada ya kupoteza muda mwingi katika kutengeneza kanuni za uendeshaji wa chombo hicho.
Wanaharakati wavamia
Wakati kamati zikijiandaa kuanza mjadala, wanaharakati wawili walivamia kwenye ukumbi wa Royal Village, wakiwa na mabango yenye maandishi yanayowataka wajumbe kutetea maoni ya wananchi yaliyomo kwenye rasimu ya Katiba.
Hata hivyo, watu hao baadaye waliondolewa kwenye eneo la hoteli hiyo na maofisa wa
usalama majira ya saa 2:00 asubuhi.
Hata hivyo, mwenyekiti wa Kamati Namba 9, ambayo inafanya vikao vyake kwenye hoteli hiyo, Kidawa Hamis alisema kuwa hali ni shwari kwenye kamati yake na wajumbe wanaendelea kuchambua rasimu.
Katika kumbi zilizopo kwenye Hoteli ya St. Gasper, pia watu wawili walikamatwa wakiwa na mabango yanayowataka wajumbe kutambua kwamba katiba ni mali ya wananchi na si ya wanasiasa.
Hati ya Muungano
Katika makundi karibu yote, jana kuliibuka hoja juu ya Hati ya Muungano, wajumbe wakitaka kabla ya kuanza mjadala ionyeshwe kwa kuwa ndio msingi wa hoja.

No comments:

Post a Comment