EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Thursday, March 6, 2014

HUU NDIYO MWISHO WA SOKA LA Carlos Tevez TIMU YA TAIFA


TEVEZ_IN_JUVE 






















JUZI USIKU, ‘Albiceleste’, kama inavyojulikana Timu ya Taifa ya Argentina, ilitoka Sare 0-0 na Romania, Timu ambayo haipo Fainali za Kombe la Dunia, na kuonyesha dhahiri ubutu wao lakini Kocha wa Nchi hiyo hataki kusikia lolote kuhusu Carlos Tevez ambae sasa ni Supastaa huko Serie A akivurumisha Mibao kila kukicha akiwa na Klabu yake Juventus.
Kocha wa Argentina, Alejandro Sabella, amekataa kabisa kusikiza hoja yoyote ya kumwita Carlos Tevez kuichezea Nchi yake licha ya Nchi hiyo kuonyesha waziwazi wana ubutu kwenye Fowadi yao hasa baada ya kufifia Fowadi yao ya kina Lionel Messi, ambae kwenye Mechi hiyo na Romania alikuwa akitapika Uwanjani, huku Sergio Aguero, Gonzalo Higuain, Rodrigo Palacio na Ezequiel Lavezzi wakiwa ni magoigoi tu.
Akiwa na Juve Msimu huu, Carlos Tevez ametoboa nyavu mara 15 na anaonyesha ni mpiganaji hodari lakini Alejandro Sabella hataki kusikiza lolote.
Alipohojiwa kuhusu Tevez, Alejandro Sabella, alijibu: “Nina imani na Wachezaji wangu na nawaamini Mastraika wangu. Wote ni Nyota wa Argentina. Sitaki kuzungumzia Mchezaji yeyote ambae hayuko hapa.”
Tevez, mwenye Miaka 29, hajaitwa Timu ya Taifa ya Argentina tangu Kocha Alejandro Sabella ateuliwe wadhifa huo Agosti 2011.
Mwezi Desemba Tevez aliwahi kutamka: “Kama Sabella hajaniita siwezi kumpigia Simu na kumuuliza kwanini hakunichagua. Sabella asiombwe kunichukua…mwacheni afanye kazi yake kwa amani kwa sababu si rahisi Sabella kuniacha mimi. Najua ipo presha kubwa toka kwa Mashabiki.”
Tevez, ambae amewahi kuzichezea Klabu za England za Manchester City, Manchester United na West Ham, amesema yeye ana uhusiano mzuri na Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Argentina pamoja na Nahodha wake Lionel Messi.
Tevez alisema: “Sina tatizo na kundi lile na naelewana vizuri mno na Messi. Sipotezi usingizi kwa sababu ya Kombe la Dunia. Sidhani kama nitaitazama kwa sababu inauma kuiona Timu ya Taifa, ni mbaya kwangu!”
Mara ya mwisho kwa Tevez kuichezea Argentina ni kwenye Robo Fainali ya Copa America ya Mwaka 2011 ambapo Argentina ilifungwa na Uruguay.
Pia Tevez alikuwemo Kikosi cha Argentina kilichocheza Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2006 huko Germany na Afrika Kusini 2010 ambako mara zote ilitolewa Robo Fainali.
Argentina, ambao wametwaa Kombe la Dunia Mwaka 1978 na 1986, kwenye Fainali za Kombe la Dunia za Brazil Mwakani wapo Kundi F pamoja na Bosnia, Iran na Nigeria.

No comments:

Post a Comment