EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Sunday, January 26, 2014

LIPUMBA APIGWA MKWARA NA CCM

Mkiti WA CUF PROF:IBRAHIM LIPUMBA
JUMUIYA ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) imemuonya Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) Taifa, Profesa Ibrahim Lipumba kuacha kuingilia uamuzi wa kikatiba unaofikiwa na chama hicho.
Hivyo wamemtaka kushughulikia maendeleo ya chama chake na kuwaeleza wananchi nini chama chake kitafanya ikiwa mgombea wa chama hicho atashinda katika nafasi ya uwakilishi jimbo la Kiembesamaki.
Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM Zanzibar, Shaka Hamdu Shaka alisema hayo wakati akimnadi mgombea wa nafasi ya uwakilishi jimbo la Kiembesamaki, Mahmoud Thabit Kombo katika eneo la Buyu Kisiwani Unguja .
Shaka alikipuuza kitendo cha Mwenyekiti huyo wa CUF aliyetaka CCM kama ina ubavu, iwafukuze wanachama wake watatu wanaotetea mfumo wa serikali tatu, wakiwemo mawaziri wakuu wastaafu, Dk Salim Ahmed Salim na Joseph Warioba na mwanasiasa mkongwe, Joseph Butiku.
HABARI LEO

No comments:

Post a Comment