SERIKALI imeamua kupunguza kwa kiasi kikubwa bei ya kuunganisha umeme majumbani
na kufikia sh. 27,000/ kwa wanavijiji wanaoishi kwenye maeneo ambayo bomba la
gesi linapita.
Hatua
hiyo imetangazwa jana (Jumapili, Januari 26, 2014), na Waziri wa Nishati na
Madini, Prof. Sospeter Muhongo wakati akizungumza na wanakijiji wa Mangaka
wilayani Nanyumbu, mkoani Mtwara kabla ya kumkaribisha Waziri Mkuu, Mizengo
Pinda azindue mradi wa umeme kwenye wilaya hiyo.
“Jana
Waziri Mkuu aliagiza tutafute namna ya kuwasaidia wananchi wanaoishi jirani na
njia ya bomba la gesi. Nami nilikaa na wasaidizi wangu jana usiku na kufanya
hesabu na tukaamua tuweke kiwango hicho kwa ajili ya wakazi hao,” alisema.
Alisema
katika mikoa mikoa mingine gharama za kuunganisha umeme ni sh. 177,000/- lakini
kwa mikoa ya Lindi na Mtwara gharama hizo zilishushwa na kufikia sh.99,000/-.
“Lakini sasa hawa wenzetu tumewapa upendeleo zaidi na tumewapunguzia gharama
hizo hadi sh. 27,000/-,” alisema huku akishangiliwa.
No comments:
Post a Comment