EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Wednesday, November 6, 2013

NSSF YATOA WITO KWA MADAKTARI NA WAUGUZI MKOANI MTWARA KUJALI UTENDAJI



Madaktari na wauguzi mkoani Mtwara wametakiwa kutoa ushirikiano na huduma bora kwa wagonjwa waliojiunga na mfuko wa hifadhi ya jamii wa (NSSF) Mkoani Mtwara.
moja kati ya wagonjwa akiwa amelazwa katika Hospitali ya Ligula Mtwara
 Wito huo umetolewa na meneja wa mfuko wa huo mkoa wa Mtwara Stanley Millanzi , wakati akizungumza na mwandishi wa habari wa kituo hiki mapema leo ofisini kwake.
Millazi amesema kuwa kwa wananchama waliojiunga na mfuko huo, wanaweza kupata huduma ya afya kwenye vituo vilivyo karibu na maeneo wanayoishi.Amezitaja sehemu zinazotoa huduma kwa wanachama hao kwa Mkoa wa Mtwara, ambazo ni hospitali ya Rufaa ya Ligula pamoja na ndanda ndogo zote katika Manispaa ya Mtwara ya Mikindani.
Aidha Millanzi amesema wanachama wa mfuko huo wanaweza kupata huduma hiyo katika vituo vingine vya afya vinavyotoa huduma hiyo, ikiwa ni pamoja na hosiatali ya Busa ,Mkomaindo ,Nanyumbu, pamoja na hospitali ya wilaya ya tandahimba.

No comments:

Post a Comment