EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Wednesday, November 6, 2013

MAN CITY YAPIGA MTU TANO KWAO , MAN UNITED YASHIKWA ULAYA

MABAO ya Sergio Aguero na Alvaro Negredo yametoa mchango mkubwa wa ushindi wa Manchester City 5-2 dhidi ya CSKA ya Urusi katika Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku huu na kuifanya klabu hiyo ifuzu kwa mara ya kwanza kutoka hatua ya makundi ya michuano hiyo katika histoeia yake.
Aguero alifunga bao la kwanza kwa penalti dakika ya pili baada ya David Silva kuangushwa kwenye eneo la hatari na Zoran Tosic.

Mshambuliaji huyo wa Argentina akafunga la pili dakika 10 baadaye, kabla ya Negredo kufunga la tatu dakika ya 30 pasi ya Aguero, la nne dakika ya 51 pasi ya Samir Nasri na la tano dakika ya pili ya muda wa nyongeza baada ya kutimia dakika 90, pasi ya James Milner.
Mabao ya CSKA yamefungwa na Doumbia dakika ya 45 pasi ya Wernbloom na dakika y 71.


Sealed with a kiss: Aguero wheels away to the Manchester City supporters at the Etihad
Huko nchini hispania Robin van Persie alikosa mkwaju wa penalti na kiungo Marouane Fellaini akilimwa kadi nyekundu huku Manchester United ikijiweka kwenye nafasi ya kufuzu hatua ya 16 bora pale ilipolazimishwa sare ya bila kufungana na Real Sociedad.
Paris St Germain walilazimishwa sare ya bao 1-1 nyumbani na Anderlecht ya Ubelgiji kwenye mchzeo wa kundi C.
Wageni walitangulia kufunga dakika 20 kabla ya mchezo kumalizika kupitia kwa Demy De Zeeuw kabla ya Zlatan Ibrahimovic hajafunga bao la kusawazisha dakika mbili baadae.


Real Madrid walinyimwa nafasi ya kufuzu hatua ya 16 bora ya Champions League hapa jana  usiku baada ya kulazimishwa sare ya mabao 2-2 d kwenye mchezo wa kuvutia dhidi ya Juventus.
Ushindi nchini Italia ungeivusha Real Madrid kwenye hatua inayofuata.


Sare ya jana imewapa matumaini Juventus ya kufuzu kutoka kundi B hasa baada ya FC Copenhagen kuifunga Galatasaray 1-0.Mario Mandzukic aliifungia bao pekee Bayern Munich kwenye ushindi wa bao 1-0 ugenini dhidi ya Plzen,ushindi huo uliakikishia nafasi Bayern kufuzu hatua ya mtoani 


No comments:

Post a Comment