NA SHAFII MOHAMEDI ,ARUSHA
Timu ya soka ya
wachezaji wa zamani Arusha All star veterans leo imekiona cha moto baada
ya kulambishwa kipigo cha mabao manne
4-0 kutoka kwa timu ya soka ya mamlaka ya mapato TRA Mkoa huu wa Arusha kwenye bonanza la kuazimisha siku ya mlipa
kodi ndani ya uwanja wa kumbukumbu ya
shekhe Amri Abeid
Bonanza hilo ambalo limefanyika kuanziamajira ya saa nne za
asubuhi limeshirikisha timu nne za mpira
wa miguu ambazo ni Ilboru secondary ,Arusha secondary ,Arusha All star pamoja na timu ya TRA huku
zikishindana kwenye michezo ya soka, kuvuta kamba na kukimbiza kuku
Katiaka mchezohuo jahazi la All star lilianza kuzama kipindi cha
kwanza baada ya Mchezaji Mkope Geoge
kuanza kuifungia TRA goli dakika ya tatu ya mchezo wakati la pili likiwekwa kimiani na Ruben
Abel na kufanya TRA kumaliza kipindin cha kwanza wakiwa mbele kwa mabao 2-0
Kipindi cha pili kimeanza kwa All star kuonyesha uhai wa
kurudisha magoli hayo lakini haikuwa hivyo baada ya mchezaji Hosea Mangwa
kukwamisha wavuni goli la tatu wakati kalamu ya magoli katiak mtanange
huo ilihitimishwa na mchezaji Said
Mwamloso na kufanya matokeo kuwa 4-0
TRAwaliokuwa wakiongozwa na mchezaji wa zamani Rashid Idd chama wameweza kuwa mabingwa wa bonaza hilo kwa upande wa soka na kukimbiza
kuku wakati All star wamekuwa washindi kwenye
upande wa kuvuta kamba pekee
Mchezo wa kwanza ambo
umechezwa mapema sana uliozikutanisha
Arusha sekondari dhidi ya shule
ya sekondari ya ILBORU imeshuhudiwa ilboru ikiibika na ushindi wa 2-0 kwa magoli ya
Daniel maugo wa kidato cha sita na goli la pili likiwekwa kimiani na Fidelis
Mkanga wa kidato cha 3 laskini kwa upande wa net ball mira wa mikono kwa wasichana
Arusha sec wameweza kuwa tandika
Mateve sekondari 16-6
Maazimishon ya siku hii ya mlipa kodi yameanza Nov mosi na
yanatarajiwa kufikia kilele Nov 8 ya
mwaka huu kwa taifa zima kuazimisha siku ya mlipa kodi
No comments:
Post a Comment