EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Thursday, February 27, 2014

WAJUMBE WA BUNGE LA KATIBA WAPIGWA KUFULI KAULI ZA KIITIKADI NDANI YA BUNGE HILO JAJI MIHAYO ASEMA HAKUNA UBINAFSI WA KISIASA KWA FAIDA YA WACHACHE KWENYE MASLAHI YA TAIFA LA WOTE


Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani,Thomas Mihayo.
Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani, Thomas Mihayo ametoa rai kwa wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, viongozi wa umma na viongozi wa siasa, kujiepusha na kauli na mienendo ya itikadi za vyama vya siasa na maslahi binafsi ya makundi machache katika kujadili rasimu ya Katiba.
Pia amewataka kutambua kwamba wametumwa Dodoma na wananchi kuwapatia Watanzania Katiba bora na si kutimiza matakwa ya watu wachache.

Alitoa rai hiyo jijini Dar es Salaam jana wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kitaifa ya kusambaza uelewa wa rasimu ya Katiba kwa wananchi inayotambukila kama  “Big  Bang Constitutional Campaign (BBCC) iliyoandaliwa na asasi za kiaraia (Azaki) na kuratibiwa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC).

Alisema mchakato wa Katiba si wa wanasiasa, wanasheria wala wasomi pekee, bali ni wa wananchi wote, hivyo wanapaswa kushirikishwa katika kila hatua.


 “Ikiwa  Katiba inayopendekezwa itakuwa bora, basi wananchi watakuwa na shauku ya kushiriki kikamilifu katika kura ya maoni ili kujipatia Katiba inayofaa na si vinginevyo.
Tunatambua kuwa katika kipindi hiki cha mpito, kila kundi na kila kiongozi atawajibika kwa mwenendo, kauli au matendo kuhimiza chuki, fujo, vurugu au uvunjifu wa amani kwa njia yoyote” alisema.
Pia Jaji Mihayo alitoa wito kwa viongozi wa dini na vyama vya siasa kuhimiza wafuasi wao kujali zaidi maslahi ya taifa kuliko maslahi mengine.

CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment