EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Tuesday, November 5, 2013

AFC BINGWA LIGI YA TAIFA JIJI LA ARUSHA

NA   Shafii Mohamed ,Arusha
Timu ya soka ya  AFC leo imetawazwa kuwa bingwa mpya michuani ya ligi ya taifa ngazi ya wilaya  ya Arusha mjini kwa kujikusanyia jumla ya pointi10 katika hatua ya 6 bora  ligi ambayo imeanza  mnamo mwezi wa 7 kwa kushirikisha jumla ya timu 18 za jiji la Arusha.

michuano hiyo ambayo imefikia tamati leo kwa michezo mitatu  ilio pigwa katika viwnja tofauti ,uwanja wa engutoto  watoto wa mchezaji wa zamani rashid idd chama CIDT SC wametoka sare ya bila kufungana  0-0 dhidi ya SUYE SC hivyo kuifanya suye kushika nafasi ya pili kwa kujikusanyia pointi 7 katiaka round hii.

Katika uwanja wa shule ya sekondari ya ILBORU  AFC wamepokea kipigo cha  1-0 kutoka kwa timu ya jeshi 977fc lakini kipigo hicho hakikuweza kuivua ubingwa AFC ambao tayali wamekwisha jihakikishia  ubingwa huo kwa kushinda michezo mitatu na kutoa sare mchezo mmja na kufungwa mechi m0ja katika hatua ya 6 bora

Mchezo wa mwisho uliwakutanisha NYOTA SC almaarufu brazil wa Arusha kutoka maeneo ya daraja2  dhidi ya MALTI FLOWER FC  katika awanja wa kukmbukumbu ya shekhe Amri Abeid  na timu hizo kutoka sere ya kufungana  1-1  lakini sare hiyo ilikuwa balaa kwa timu zote mbili

Mbali na kuwa binngwa leo ikumbukwe AFC ilifanya vizuri sana katika hatua ya makundi   kwa kumaliza ikiwa imejiksanyia pointi 16

Akizungumza na swacotz katibu wa chama cha mpira  wilaya ya Arusha mjini Zakayo mjema amethibisha kuwa kwa matokeo hayo AFC pamoja n suye sc ndio timu ambazo zita wakirisha jiji la Arusha katika michuano ya ligi ya mkoa ambayo itaanza hivi karibuni
 


No comments:

Post a Comment