EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Friday, October 18, 2013

CHAMA CHA MSINGI CAH USHIRIKA NACHINGWEA CHASHITAKIWA CHADAIWA MIL 22.9



Wakulima 26 wa kata za Nambambo na Nachingwea, Wilaya ya Nachingwea, Mkoa wa Lindi wamefungua kesi ya madai wakitaka Chama cha Msingi cha Ushirika cha Nambambo, kuwalipa Sh milioni 22.9 zilizosalia kutokana na malipo ya mauzo ya zao la korosho za msimu uliopita, 


ambapo walilipwa pungufu ya bei dira waliyokubaliana.
Katibu wa kamati inayofuatilia madai hayo, Ahmadi Majali amesema kuwa wakulima hao wamefungua mashtaka hayo katika Mahakama ya Wilaya ya Nachingwea wakitaka chama hicho kiwalipe kiasi hicho cha fedha zilizosalia kutokana na malipo ya korosho zenye uzito wa kilo 163,947 zenye thamani ya Sh milioni 77.2 walizokiuzia chama hicho msimu uliopita.


Majali amesema kuwa wamefikia uamuzi huo baada ya juhudi za kutaka suala hilo kumalizwa nje ya mahakama kushindikana, huku kukiwa hakuna dalili zozote zinazoonyesha kuwa zitalipwa wakati msimu mpya wa mauzo ya zao hilo ukiwa umeanza.Kwa upande wake Mwenyekiti wa chama hicho cha ushirika cha msingi cha Nambambo, Sadiki Kachambila amekiri chama chake kufikishwa mahakamani wiki ijayo, na kudai kuwa wao walikuwa ni mawakala na wa mazao kwa wakulima na kuwa wanaostahili kufikishwa mahakamani ni chama kikuu cha Ilulu.
 

No comments:

Post a Comment