- ASISITIZA WALIPWE NDANI YA MIEZI SITA
- ASEMA ATAKOMESHA UMANGI MEZA WA WATUMISHI WA CHAMA NA SERIKALI
- AWAAMBIA WAKAZI WA KATA YA KIBARA WANACHOITA KIWANDA SI KIWANDA BALI NI GOFU
- ASISITIZA KAMA MTU HAWEZI KAZI AONDOKE MWENYEWE
- ATAKA KUIREJESHA CCM YA NYERERE
- NAPE ASHANGWAZWA NA WANAOLIVALIA NJUGA SUALA LA BALOZI WA CHINA
- ASEMA MSAJIRI KASHAURIWA VIBAYA
Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana akipokelewa kwa gwaride nadhifu la chipukizi wa mkoani Mara.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na Ndgugu Stephen
Wassira mara baada ya kukagua mradi wa kusambaza maji kwa wilaya ya
Bunda
Katibu
Mkuu wa CCM akipokelewa na wananchi wa kata ya Kibara katika jimbo la
Mwibara alipotembelea kuona jinsi ilani ya uchaguzi inatekelezwa.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikata utepe kuashiria kufungua
kwa mradi wa kujenga chuo cha ufundi fundi Stadi katika jimbo la Mwibara, kulia ni mbunge ndugu Kange Ligora na kushoto ni mwenyekiti wa CCM mkoa ndugu Christopher Sanya.
Katibu
Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana akimimina zege kwenye
shughuli za ujenzi wa chuo cha Veta cha Namibu ambacho ni sehemu ya kazi
nzuri ya mbunge wa Mwibara Ndugu Kange Lugora.
Mbunge
wa Ludewa akisalimiana na wananchi wa kata ya Kibara ambapo alitoa
pongezi kwa ujenzi wa chuo cha ufundi na kuongeza nguvu akachangia
mabati mia tano pamja na siment mifuko mia moja.
Katibu
Mkuu wa Umoja wa Wanawake nchi Ndugu Amina Makilagi akisalimia wakazi
wa kata ya Kibara , akingea ujumbe mmoja tu alisema wakazi wa Bunda
acheni kuua wakina mama wazee kwa tuhuma za uchawi alichukua nafasi hiyo
kukaa kama wanandugu na kukomesha kabisa mauaji hayo .
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongea na wananchi wa jimbo la
Mwibara na kuwaambia maendeleo hayaji kama mvua kwa siku moja ni muhimu
kushikamana na kushirikiana na viongozi wao katika kutatua na kuleta
maendeleo yao.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongoza maandamano ya kuelekea
kwenye viwanja vya mkutano baada ya kufungua shina la wajasriamali
wakereketwa wa Pamba road.
Mbunge
wa Bunda na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais ( Mahusiano na Uratibu)
akihutubia wakazi wa Bunda kwenye mkutano mkubwa wa CCM uliokuwa
unaongozwa na Katibu Mkuu wa CCM
Mbunge
wa Ludewa Ndugu Deo Filikunjombe akiwasalimu wananchi wa Bunda wakati
wa mkutano wa hadhara ambao Katibu Mkuu alihudhuria.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wananchi wa wilaya ya Bunda waliofika kusikiliza mkutano huo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia umati wa watu uliojazana kumsikiliza katika viwanja vya Bunda.
Katibu Mkuu wa CCM akikabidhiwa zawadi za kumtambulisha kama Mzee wa wilaya ya Bunda.
Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akitoa mkono wa shukrani baada ya
kukabidhiwa zawadi za heshima kama Kijana wa Wilaya ya Bunda.
**************************
Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana anaendelea
na ziara yake na sasa ameingia katika Mkoa wa Mara na tayari ametembelea
shughuli za utekelezaji wa ilani ya uchaguzi katika wilaya ya Bunda.
Katika ziara hiyo Katibu Mkuu alianza kwa kupokea taarifa
ya hali ya kisiasa wilayani hapo na kisha kutembelea mradi wa maji ambao
umekuwa ukilalamikiwa muda mrefu kuwa unachukua muda kukamilika,katika mradi
huo amekuta hatua ya kwanza kuwekwa kwa bomba kubwa umeanza ,pia alipata nafasi
ya kutembelea jimbo la Mwibara ambapo alishiriki katika ujenzi wa madarasa ya chuo cha ufundi stadi Namibu
na kutembelea shule ya Sekondari Mwibara katika kata ya Kibara pamoja na
kutembelea kiwanda cha Mara Coooperative 1984.
Ziara hiyo wilayani Bunda ilihitimishwa kwa mkutano wa
hadhara ambao ulijaza umati si wa kawaida.
Katika Mkutano huo Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape
Nnauye alisema tangia Kinana
amechaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa CCM Mabalozi karibia nusu wamekuwa wakifika
ofisini kumpa pongezi bila kificho na kuonyesha kufurahishwa kwao kwa uteuzi
huo “Nawashangaa watani zetu kukomalia suala la balozi wa China wakati huu
wakati ambao tumefanikiwa kupata ufumbuzi
wa matatizo ya wakulima wa Pamba”,aliendelea kusema mabalozi wamekuwa
wakishiriki kwenye shughuli mbalimbali za CCM ikiwemo kuwa wageni waalikwa
kwenye mikutano mikuu ya CCM na hiyo yote haijawahi leta maneno, Akasema msajiri
wa vyama ameshauriwa vibaya kuhusu hili.
Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana ameendelea
kusisitiza juu ya madai ya walimu nchi nzima kulipwa kwa wakati bila kuwa ya
malimbikizo,alisema tatizo hili la muda mrefu na Rais alishatolea maagizo lakini halitekelezwi akasema kama Katibu Mkuu
wa Chama anatoa miezi sita walimu wawe wamelipwa madai yao na kama
halitofanyika yeye kama Katibu Mkuu atalipeleka kwa wabunge wa CCM kasha wapitishe
azimio Bungeni la kufukuzwa kazi wahusika.
Katibu Mkuu alisema “ watu wamekaa mjini wanalipwa
vizuri, magari mazuri na suti wamevaa lakini hawajali wenzao wanajilipa posho
kila kikao”
Katibu Mkuu alisisitiza kuwa anamuomba Waziri Mkuu azuie
vikao wakati wa kazi na vikao vyote vifanyika baada ya muda wa kawaida wa kazi
kumalizika.
Alisisitiza yeye ni Katibu Mkuu wa CCM anayefanya kazi
kwa vitendo na amedhamiria kuhakikisha chama kinafanya kazi nzuri ya kuiongoza
seri
No comments:
Post a Comment