MTOTO Ashura Mustapha (7) mkazi wa Mwandege, wilayani Mkuranga, Pwani
anasumbuliwa na ugonjwa wa kansa ya ngozi tangu akiwa na mwaka mmoja.
Akizungumza na mwandishi wetu, baba mzazi wa mtoto huyo, Mustapha
Makombe alisema: “Mwanangu anateseka sana jamani, ugonjwa ulianza kama
malengelenge akiwa na umri wa mwaka mmoja tukawa tunakwenda hospitali
ndogondogo lakini baadaye tukaamua kumpeleka Muhimbili ambapo tulipewa
barua ya kutuelekeza kwenda CCBRT, kule ndipo wakagundua mwanangu ana
kansa ya ngozi steji ya nne.
“Baada ya kuhangaika katika hospitali
nyingi bila mafanikio, nikaamua kwenda Hospitali ya Regency (Dar) kuomba
msaada...
MASAA 48 WALIYOPEWA WAASI WA M23 YAKO UKINGONI.....KICHAPO KITAANZA MUDA WOWOTE
Muda wa saa 48 wa kusalimisha silaha kwa waasi wa March
23(M23), Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo umemalizika na
wakati wowote mapigano yanaweza kuanza.
Misheni ya Kutuliza Amani ya Umoja wa
Mataifa(Monusco) , ilitoa saa hizo zinazomalizika leo na Jeshi la UN
litaanza kutumia nguvu kunyang’anya silaha waasi hao.
Taarifa ya Monusco iliyotolewa na
Msimamizi wa Misheni hiyo, Luteni Jenerali Carlos Alberto dos Santos
Cruz na kusambazwa na Idara ya Mawasiliano ya Umoja wa Mataifa jana,
inaeleza kwamba, watu binafsi katika eneo la Kivu ya Magharibi...
No comments:
Post a Comment