EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Saturday, July 20, 2013

VIONGOZI WA CHADEMA WAKITOA SADAKA YA SHUKRANI ARUSHA

Siku ya leo, CHADEMA mkoa wa Arusha walikuwa na ratiba muhimu ya Kutoa sadaka ya shukurani kwa Mungu kwa kutembelea vituo vya watoto yatima na wenye mahitaji muhimu na kuwapa misaada ya vitu mbalimbali na fedha taslimu kufuatia baraka za Mungu kuwawezesha baadhi kunusurika kifo kwa mabomu na pia kwa ushindi mnono.

Msafara wa CHADEMA ulikuwa na viongozi wa chama wakiongozwa na mwenyekiti wa chama Wilaya aliyewakilisha pia mkoa, pamoja na madiwani wapya bila kuwasahau viongozi wa BAVICHA na makamanda Ally Bananga na Alphonce Mawazo.

Vitu vyote walivyotoa msaada kama sadaka vimetokana na michango binafsi ya wanachama na wapenzi wa CHADEMA zikiwemo familia kadhaa zilizoamua kuungana na chama katika sadaka hiyo.

Vituo vilivotembelewa ni cha Abu-Abdurahaman Oprhanage Centre cha Mbauda ambacho kinapoke a watoto wa kuanzia miaka mitatu na Samaritan Village cha Moshono ambacho kinapokea watoto wachangakabisa kuanzia chini ya mwezi mmoja, na wengi ni wale wanaotupwa na wazazi wao vichakani au majalalani na kwenye mifuko mara baada ya kujifungua.













Mkutano wa CHADEMA mkoa wa Shinyanga leo






No comments:

Post a Comment