Kesi ya mauaji ya Padri Evarist Mushi imechukua sura mpya, kufuatia
Jaji wa Mahakama kuu ya Zanzibar, Mkusa Isaac Sepetu kujitoa baada ya
upande wa utetezi kuwasilisha ombi la mshatikiwa Omar Mussa Makame
kutokuwa na imani naye.Akisoma uamuzi baada ya kupokea maombi ya
upande wa utetezi, ambayo yaliwasilishwa Julai 2 mwaka huu, Jaji Mkusa
amesema kwamba uamuzi wa mshtakiwa ni haki yake kwa mujibu wa sheria
lakini amesema hakubaliani na hoja zilizotolewa na Wakili Abdallah Juma
Mohamed.
Wakili Abdallah Juma Mohamed aliwasilisha hoja tatu,
akimtaka Jaji Mkusa ajiondoe katika kesi hiyo, kuutaka upande wa
waendesha mashtaka wapewe...
MWENYEKITI WA HALMASHAURI AFARIKI DUNIA BAADA YA KUANGUKA CHOONI
MWENYEKITI wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma,
Laurent Hoya, amefariki dunia ghafla jana alfajiri baada ya kuanguka
chooni. Kifo hicho kimetokea nyumbani kwa marehemu Nkuhungu katika
Manispaa ya Dodoma.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi jana, Mkuu wa Wilaya ya
Chamwino, Fatma Ally alisema Hoya ambaye alikuwa na tatizo la ugonjwa wa
moyo, alianguka chooni jana alfajiri na kukutwa na mauti.
“Tuliachana juzi saa 7.30 mara baada ya kikao, taarifa ya kifo chake
nilizipata saa 11 alfajiri jana, ni kifo cha ghafla sana na halmashauri
imempoteza mtu ambaye alikuwa mfano kwa jamii,” alisema.
Hoya ambaye alikuwa Diwani wa Kata ya Mpwayungu, anatarajiwa kuzikwa kijijini kwake Mpwayungu kesho.
Mkuu huyo wa Wilaya alisema alikuwa akishirikiana kwa karibu na
Mwenyekiti...
KWA NINI CCM IKIHOFIE CHADEMA??
TANGU kuanzishwa kwa vyama vingi nchini mwaka 1992, tayari chaguzi nne
zinazoshirikisha vyama vingi zimefanyika.
Katika chaguzi hizo nne, Chama
Cha Mapinduzi (CCM), kimeendelea kushika dola kwa ushindi wa kishindo
katika kiti cha urais, wabunge na madiwani.
Ushindi huu wa kishindo
umeendelea kupungua kutoka ngazi ya ubunge na udiwani, ambapo wapinzani
wamekuwa wakinyakua viti vya majimbo hata ambavyo vilikuwa vinatajwa
kuwa ngome ya CCM.
Kupungua huko kwa viti vya ubunge na udiwani, ni kiashiria kuwa
huenda kwa mara ya kwanza katika historia ya uchaguzi nchini, CCM
itaenda katika uchaguzi mkuu mwaka 2015, kikiwa...
NAPE AKWEPA KUZUNGUMZIA MATOKEO UDIWANI ARUSHA..."WAULIZENI VIONGOZI WA CCM ARUSHA"
Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC), Itikadi na Uenezi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye
Katibu
wa Halmashauri Kuu (NEC), Itikadi na Uenezi ya Chama Cha Mapinduzi
(CCM), Nape Nnauye, amesema wanaopaswa kuulizwa jambo lolote linalohusu
uchaguzi wa udiwani wa kata nne uliofanyika Jumapili wiki iliyopita,
jijini Arusha, ni viongozi wa chama wa mkoa huo.
Nape alisema
hayo alipozungumza na Nipashe jijini Dar es Salaam jana, baada ya
kutakiwa kutoa maoni yake kufuatia Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema) kuibuka mshindi katika kata zote nne.
“Waulize
wenyewe. Siwezi kuzungumzia issue (suala) ndogo. Unajua...
No comments:
Post a Comment