EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Monday, July 1, 2013

HAMILTON AITAKA PIRELLI KUCHUKUA HATUA ZA HARAKA KUHUSIANA NA MAGURUDUMU YAO KABLA MADHARA MAKUBWA HAYAJATOKEA.


DEREVA nyota wa magari yaendayo kasi ya langalanga kutoka timu ya Marcedes, Lewis Hamilton amesema kampuni ya magurudumu ya Pirelli inatakiwa kuchukua hatua mapema baada ya magurudumu kuharibika vibaya katika mashindano ya British Grand Prix. Madereva wanne walipasukiwa na matairi katika mashindano hayo, huku Hamilton yeye akipasukiwa tairi lake katika mzunguko wa saba wakati akiongoza mbio hizo. Hamilton alitoa tahadhari kuwa hatua za haraka zinapaswa kuchukuliwa na Pirelli ili kuzuia matatizo kama hayo siku za usoni kwani inaweza kuwa hatari zaidi hata kufikia watu kupoteza maisha. Katika mbio hizo Hamilton alishika nafasi ya nne huku dereva mwenzake wa timu ya Marcedes Nico Rosberg akishinda mbio hizo na kufuatiwa na Mark Webber wa Red Bull wakati nafasi ya tatu ilichukuliwa na Fernando Alonso wa Ferrari.

Sunday, June 30, 2013

VILLAS-BOAS KUSTAAFU MIAKA 10 IJAYO.

MENEJA wa klabu ya Tottenham Hotspurs, Andre Villas-Boas amebainisha mipango ya kustaafu kufundisha wakati atapofikisha miaka 45. Kocha huyo mwenye miaka 35 raia wa Ureno amekuwa kocha mdogo zaidi kushinda taji la Europa League wakati akiwa na klabu ya Porto miaka miwili iliyopita, kabla ya kwenda Chelsea ambako alitimuliwa kwa kushindwa kufanya vyema na kwenda Spurs alipo sasa. Pamoja na kwamba Villas-Boas amesisitiza kuwa anafurahia kazi hiyo ya ukocha lakini haoni kama atafanya shughuli hiyo kwa kipindi kirefu kama makocha wengine. Villas-Boas amesema amapenzi yake katika soka yanamfanya aishi maisha ya wasiwasi kwa kipindi cha miezi 11 katika mwaka na anadhani maisha yamruhusu mtu kufurahia vitu vingine zaidi ndio maana ameamua baada ya miaka 10 ijayo atastaafu rasmi shughuli hiyo. Kocha huyo aliendelea kudai kuwa amekuwa na ndoto za kipindi kirefu kushiriki mashindano ya Dakar Rally hivyo akiachana na mambo ya ukocha ataelekeza shughuli zake katika mashindano hayo yenye historia ya kipekee duniani. 

WILLIAMS, DJOKOVIC WAENDELEA KUPASUA ANGA WIMBLEDON.

MWANADADA nyota wa mchezo wa tenisi kutoka Marekani, Serena Williams amefanikiwa kuingia katika mzunguko wan ne wa michuano ya Wimbledon baada ya kumuengua Kimiko Date-Krumm wa Japan katika mzunguko wa tatu wa michuano hiyo. Williams ambaye anashika namba moja katika orodha za ubora duniani na bingwa mtetezi wa michuano katika mchezo huo alimshinda Krumm kwa 6-2 6-0 akitumia muda wa dakika 61 pekee. Krumm mwenye umri wa miaka 42 amekuwa mwanamke mwenye umri mkubwa zaidi kuingia mzunguko wa tatu wa michuano hiyo inayoendelea jijini London, Uingereza. Kwa upande wanaume Novak Djokovic wa Serbia naye amefanikiwa kutinga hatua ya 16 bora baada ya kumtandika Jeremy Chardy wa Ufaransa kwa 6-3 6-2 6-2.

No comments:

Post a Comment