EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Thursday, July 18, 2013

DR.KIKWETE:WALIOHUSIKA NA MAUAJI SUDANI KUTIWA MBARONI


Rais Jakaya Kikwete amefanya mazungumzo kwa njia ya simu na Rais wa Sudan, Omar Bashir, kuhusu kuuawa na kujeruhiwa kwa askari wa Tanzania, walioko katika ulinzi wa kimataifa wa amani katika jimbo la Darfur. Taarifa ya Ikulu iliyotumwa kwa vyombo vya habari jana, imeeleza kuwa katika mazungumzo hayo, Rais  Kikwete alimtaka Rais Bashir kuchukua hatua za haraka kuwasaka na kuwakamata waliohusika na kitendo hicho kiovu, na kuwafikisha mbele ya sheria haraka iwezekanavyo. Rais Bashir amekubaliana na Rais Kikwete na kumuahidi kuwasaka hadi kuwakamata wale wote waliohusika na kuwachukulia hatua za kisheria. Alimueleza Rais Kikwete...

MZEE MANDELA ASHEREHEKEA MIAKA 95 LEO HUKU AKIWA MAHUTUTI HOSPITALINI

Afrika Kusini leo wanasherehekea miaka 95 ya kuzaliwa kwa Mzee Nelson Mandela huku rais huyo wa zamani bado yuko mahututi hospitalini. Ilikuwa ikitabiriwa kwamba shujaa huyo wa vita dhidi ya ubaguzi wa rangi kwamba angeruhusiwa kwenda kusherehekea siku yake ya kuzaliwa lakini bado yuko hospitali kutokana na kurejea maambukizi kwenye mapafu. Kituo cha Kumbukumbu ya Nelson Mandela na makundi mengine yamewataka watu kujitolea kwa dakika 67 kwa kazi za hisani kukumbukia miaka 67 ambayo Mandela aliitumikia jamii yake. Umoja wa Mataifa pia umetambua mapambano ya Mandela dhidi ya ubaguzi wa rangi na kusema siku yake ya kuzaliwa ni fursa...

No comments:

Post a Comment