KLABU
ya Barcelona ya huko Spain, katika hatua ya kushangaza, imempeleka Rais
wa La Liga Javier Tebas Mahakamani wakilalamikia kauli zake kufuatia
Mechi yao waliyoshinda kwa mbinde 3-2 dhidi ya Valencia.
Kwenye
Mechi hiyo iliyochezwa Wikiendi iliyopita, Valencia walipigwa Faini
EURO 1,500 baada ya Chupa ya Maji kurushwa toka Jukwaani kwa Washabiki
na kuwalenga Wachezaji Uwanjani.
Mbali
ya kushushwa Faini hiyo, Kamati ya Nidhamu ya La Liga iliponda vitendo
vya Wachezaji wa Barcelona waliposhangilia Bao lao la ushindi la Penati
ya Dakika za Majeruhi iliyofungwa na Lionel Messi.
Akiongea
baada ya Mechi hiyo, Rais wa La Liga, Javier Tebas, aligusia
ushangiliaji wa Wachezaji wa Barca: “Kitu kikubwa ni ile kurushwa Chupa
ya Maji lakini baadhi ya Wachezaji walifanya vitendo ambavyo hatupendi!”
Kauli
hiyo imewafanya Barcelona kumburuza Rais huyo kwenye Mahakama ya
Michezo na Rais wa Barcelona, Josep Maria Bartomeu, ameeleza: “Kuongelea
kuhusu Wachezaji kunachochea zaidi hali tete ambayo inabidi itulizwe.
Matamshi ya Tebas ni ovyo na hayastahili kutoka kwa Kiongozi wa
Michezo!”
LA LIGA
Ratiba:
**Saa za Bongo
Ijumaa Oktoba 28
2145 CD Leganes v Real Sociedad
Jumamosi Oktoba 29
1400 Sporting Gijon v Sevilla FC
1715 Deportivo Alaves v Real Madrid CF
1930 Atletico de Madrid v Malaga CF
2145 FC Barcelona v Granada CF
Jumapili Oktobo 30
1400 SD Eibar v Villarreal CF
1815 Athletic de Bilbao v Osasuna
2030 Real Betis v RCD Espanyol
2245 Las Palmas v Celta de Vigo
Jumapili Oktoba 30
2245 Deportivo La Coruna v Valencia C.F
No comments:
Post a Comment