EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Friday, August 1, 2014

WAGENI STAND UNITED WATAMBA KUZIVAA TIMU NANE KUELEKEA LIGI KUU SOKA TANZANIA BARA.

KOCHA wa wageni wa Ligi,Timu ya Stand United Emmanuel Masawe amesema atatumia michezo minane ya Kirafiki kukitambua kikosi hicho kabla ya kuanza Ligi kuu Tanzania Bara mwaka huu.
Stand United,Polisi Morogoro na Ndanda Fc zimepanda ligi Kuu Tanzania Bara Msimu huu, zikichukua nafasi ya Rhino Rangers,JKT Oljoro na Ashanti United.

Kocha huyo alisema ,kuwa atatumia mechi nane ilikutoa tathmini ya kikosi chake ambacho anaamini kitaleta upinzani zaidi ya Mbeya City mwaka jana.

Alisema Kikosi hicho kitajipima na timu za kanada ya ziwa dhidi ya  Toto Africa ya mwanza na Geita Veterani Fc,kabla ya kuja Mkoani Morogoro kucheza na Mtibwa Sugar na Polisi Morogoro kama watahitaji kupijipima nao nguvu.

Pia ,alisema watacheza na JKT Ruvu,Ndanda Fc na timu mmoja jiji Dar es Salaam na watahitimisha na Azam Fc kwenye Uwanja Kambarage mjini Shinyanga.


Alitaja pia idadi ya mechi watakazozicheza kuwa ni  michezo nane ya kirafiki kabla ya kuanza ligi kuu msimu huu,na watacheza na Geita Veterani,Toto Africa,Mtibwa Sugar,Polisi Moro,JKT Ruvu,kama Ndanda Fc watahitaji kucheza na wao watacheza nao,pamoja na Azam fc

No comments:

Post a Comment