NIMSHUKURU Mungu kwa kutuweka hai leo, hakika yeye ni mwema.
Baada ya kusema hayo niseme kwamba leo nitazungumzia umuhimu wa kuwa na katiba mpya na kuachana na hii tuliyonayo ya mwaka 1977 ambayo hakika ina upungufu mwingi na hasa kuhusiana na deni la taifa.
Baada ya kusema hayo niseme kwamba leo nitazungumzia umuhimu wa kuwa na katiba mpya na kuachana na hii tuliyonayo ya mwaka 1977 ambayo hakika ina upungufu mwingi na hasa kuhusiana na deni la taifa.
Tofauti na hiyo, ukipitia Rasimu ya Katiba Mpya kama ilivyowasilishwa bungeni na Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba, utaona kuwa imeweka ukomo wa deni hilo. Hii ni habari njema.
Hakika katiba hii ya 1977 ina mianya mingi ya ufisadi ukilinganisha na Rasimu ya Katiba Mpya ambayo kwa hakika imejaribu kuziba mianya hiyo. Katiba tunayoitumia sasa deni la taifa limezungumzwa kwa juujuu tu katika ibara ya 41 (1) na (2) ya katiba hiyo bila kufafanua udhibiti wake utakuwaje.
Ndani ya katiba hiyo serikali imepewa mamlaka makubwa ya kikatiba ya kukopa kwa niaba ya Watanzania, lakini haielekezi chochote baada ya hapo hata kama fedha hizo zinakwenda katika mambo yasiyo na masilahi kwa wananchi.

Tumeambiwa kuwa hadi kufikia Machi 2014, deni la taifa limefikia shilingi trilioni 30.6 ikilinganishwa na shilingi trilioni 23.674 Machi 2013. Kwa hesabu hizo, kila Mtanzania bila kujua zimetumikaje, anadaiwa shilingi 600,000.
Deni hilo limeongezeka kutoka shilingi trilioni 9.3 mwaka 2007/2008 hadi trilioni 30.6 mwaka 2014/2015. Ingawa kila Mtanzania anadaiwa shilingi 600,000 bila kuelezwa mchanganuo wa matumizi yake, lakini Rasimu ya Katiba Mpya inayotokana na maoni ya Watanzania, imekuja na jibu la ukopaji huu holela ambao umewabebesha mzigo mkubwa Watanzania.
Ibara ya 228 ya rasimu hiyo, imesema wazi kuwa: ”Serikali ya Tanzania itakuwa na mamlaka ya kukopa fedha ndani na nje ya Jamhuri ya Muungano kugharamia shughuli zilizo chini ya mamlaka yake.”
Fasili ya 2(a), imesema Bunge linaweza kutunga sheria ambayo itaweka masharti ya kuzingatiwa na serikali wakati wa kukopa na itaweka ukomo wa deni la taifa na madhumuni ya deni hilo. Hii ni sahihi kwa sababu wananchi ambao ndiyo walipa kodi wanapaswa kujua mkopo uliokopwa ni wakufanyia nini.

Lakini kubwa zaidi Bunge linapewa meno katika kifungu kidogo cha 2(c), ambacho kinasema Bunge litaweka utaratibu wa kutoa taarifa bungeni kuhusu mikopo na deni la taifa. Ibara ya 3(a), imebainisha wazi kuwa taarifa hiyo lazima iweke wazi kiasi cha deni lililopo na riba yake, na matumizi yaliyofanywa na yatakayofanywa kutokana na mkopo wa fedha husika, hili pia ni jambo jema sana kwa wananchi.
Mwaka 2012, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh, aliwahi kusema hoja si kuongezeka kwa deni la taifa bali ni je mikopo hiyo ilikuwa na manufaa kwa nchi?
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) wakati huo, John Cheyo alishangaa kuona deni la taifa linazidi kupaa wakati miradi iliyopangwa haina pesa. Zinakwenda wapi?
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) wakati huo, John Cheyo alishangaa kuona deni la taifa linazidi kupaa wakati miradi iliyopangwa haina pesa. Zinakwenda wapi?
Kutokana na tatizo hili la deni la taifa kutopewa ufafanuzi wowote kwa wananchi, naungana na mapendekezo ya Tume ya Warioba kwamba fedha hizo ni lazima zipate maelezo na wapewe wawakilishi wa wananchi ambao ni wabunge mle mjengonu.
Hivyo basi angalau katiba hii mpya (kama itapita kama ilivyo), hakika itaifanya serikali kukopa kwa tija ikijua itahojiwa bungeni. Ningetamani sana tufanye uchaguzi mkuu wa mwakani tukiwa na katiba hii mpya kwani CAG amekuwa akigundua upotevu mkubwa wa fedha hizi za mikopo lakini hakuna hatua ambazo tumewahi kusikia zikichukuliwa.
Naamini Bunge likipewa meno kuwabana wanaopanga matumizi ya fedha hizo za umma, nina hakika, CAG haitakuwa na kazi kubwa ya kukokotoa mahesabu au kugundua upotevu wa fedha za umma kama inavyokuwa miaka nenda rudi.
Ni lazima wabunge wapewe rungu la kuhoji deni la taifa limekopwa kwa ajili gani na waende mbali zaidi na kuonyeshwa miradi yenyewe na kama inalingana na thamani ya pesa iliyokopwa.
Ndiyo maana natoa wito kwa Ukawa kurudi bungeni na kujadiliana haya mambo ya msingi na kuhakikisha kuwa fedha za umma hazipotei tena.
Ndiyo maana natoa wito kwa Ukawa kurudi bungeni na kujadiliana haya mambo ya msingi na kuhakikisha kuwa fedha za umma hazipotei tena.
Jipu limepasuka, siwezi kuwa adui kwa kusema ukweli.
SOURCE>>>GROBAL
No comments:
Post a Comment