ENGLAND, ambayo iko Kundi D la Fainali za Kombe la Dunia pamoja na Italy, Uruguay na Costa Rica, imeandaa Mechi 3 za Kirafiki kabla ya
FA, Chama cha Soka England, kimetangaza
kuwa England itacheza na Peru Uwanjani Wembley Jijini London hapo Mei 30
na kisha Kikosi chao kitasafiri kwenda Miami, Florida kitakapopiga
Kambi ya mwisho kabla kwenda Brazil ili kujizoeza na Hali ya Hewa ya
Joto.
Huko Miami, England itacheza na Ecuador hapo Juni 4 na kufuatia Mechi na Honduras Juni 7 zote zikichezwa Sunlife Stadium.
Akiongelea Mechi hizo, Kocha wa England,
Roy Hodgson, amesema: “Nimefurahi kwa kupata Mechi hizi na maandalizi
yetu kuelekea Fainali za Kombe la Dunia kwa ujumla. Niliwaambia wazi FA
nataka Timu kutoka Marekani ya Kusini na ya Kati na wamefanikiwa
kutuletea!”
KOMBE LA DUNIA-BRAZIL 2014
England=Kundi D:
RATIBA:
-Juni 14: v Italy
-Juni 19: v Uruguay
-Juni 24: v Costa Rica
Hodgson anatarajiwa kuteua Kikosi cha
awali cha Kombe la Dunia chenye Wachezaji 30 karibu na Mei 13 na kisha
England itapiga Kambi huko Portugal kwenye Wiki ambayo itapakana na
Fainali ya FA CUP Uwanjani Wembley na Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI
itakayochezwa Lisbon, Portugal hapo Mei 24.
Baada kucheza na Peru hapo Mei 30
Uwanjani Wembley, Kikosi cha England kitapunguzwa hadi Wachezaji 23
ambayo ndio idadi inayoruhusiwa kwa Fainali za Kombe la Dunia.
Baada Mechi zake huko Miami, England
itasafiri kwenda Rio De Janeiro, Brazil ambako ndiko itakaa kabla
kusafiri kwenda Mji wa Manaus Siku 2 kabla kuivaa Italy Mjini humo hapo
Juni 14 katika Mechi yao ya Kwanza ya Kundi D.
No comments:
Post a Comment