EBENEZA MARCH 9 2014
SWACO
royal
tt
NIMO
mvuto
Friday, May 23, 2014
SIMBA MAMBO YAPAMBA MOTO UCHAGUZI MKUU WAMBURA AWEKEWA PINGAMIZI
WAGOMBEA wanaowania nafasi ya urais wa klabu ya Simba Evance Aveva na Michael Wambura wamewekewa pingamizi.
Jana ndio ilikuwa mwisho wa kuweka pingamizi kwa wagombea katika uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika Juni 29 mwaka huu.
Mbali na Wambura na Aveva, wengine waliowekewa pingamizi ni Geofrey Nyange ‘Kaburu’ anayewania nafasi ya makamu wa rais, na wajumbe wa Kamati ya Utendaji inayomaliza muda wake akiwemo Swedi Nkwabi na Joseph Itang’are ambao wanawania makamu wa rais na Ibrahim Masudi anayewania ujumbe wa Kamati ya Utendaji.
Habari za uhakika zilizopatikana jana kwenye Kamati ya Uchaguzi ya Simba, wagombea hao wamewekewa pingamizi wakipingwa wasigombee kwa sababu mbalimbali zikiwemo uadilifu.
“Mpaka sasa waliopingwa ndio hao, hapo kuna wanaotuhumiwa kuwa si waadilifu, wengine wanapingwa kwa madai kuwa walikuwepo kwenye uongozi uliopita na hawakufanya lolote sasa wanagombea tena wataisaidiaje klabu,” alisema mtoa habari kutoka kwenye kamati hiyo.
Kwa mujibu wa ratiba ya kamati hiyo ya uchaguzi, pingamizi zilizowekwa zitasikilizwa Mei 25 na uamuzi utatolewa Mei 27 kabla ya wagombea kufanyiwa usaili Mei 29.
Aidha kwa mujibu wa ratiba hiyo, matokeo ya usaili yatatangazwa Mei na Juni 2-9 kutakuwa na masuala ya kimaadili na muda wa kukata rufaa utakuwa ni Juni 2-7.
Maamuzi ya Kamati ya Maadili yatatangazwa Juni 10-12 na rufaa zitasikilizwa Juni 8-12. Juni 13-15 kutakuwa na kukata rufaa Kamati ya Rufaa ya maadili (kama zitakuwepo) na Juni 16-20 rufaa zitasikilizwa.
Maamuzi ya mwisho ya Kamati ya Rufaa ya Maadili yatakuwa Juni 21-23 na siku inayofuata orodha ya wagombea itatangazwa ikiwa ni sambamba na kuanza kampeni mpaka Juni 28, siku moja kabla ya uchaguzi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment