EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Friday, May 23, 2014

PLUIJM AWASISITIZIA YANGA KUHAKIKISHA MKWASA HAONDOKI



Kocha Hans van der Pluijm ameshauri Yanga kuhakikisha inambakiza aliyekuwa msaidizi wake, Charles Boniface Mkwasa.

Pluijm ambaye amepata mkataba wa mwaka mmoja wa kufundisha soka nchini Saudi Arabia, amewashauri Yanga kwamba Mkwasa ni kati ya makocha bora na wachapakazi.
“Kocha amesema amefanya kaiz kwa muda mrefu barani Afrika, kati ya makocha ambao amefanya nao kazi kwa uhakika ni Mkwasa.
“Amesisitiza tufanye kila linalowezekana kuhakikisha anabaki, amesema hata akija kocha yupi, basi lazima tuhakikishe anabaki pale,” alisema mmoja wa viongozi wa Yanga ambaye hakutaka kutajwa.
Pea ya Mkwasa na Pluijm imeimaliza ligi kuu ikiwa katika nafasi ya pili na tayari Yanga wameanza mchakato wa kusaka kocha mpya.

No comments:

Post a Comment