EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Sunday, May 11, 2014

Mtoto awaua kwa mapanga wazazi wake, atoweka

Kamanda wa polisi Robert Boaz.PICHA|MAKTABA 
Hai. Kijana aliyetambulika kwa jina la Yusufu Njau (32) mkazi wa kijiji cha Roo Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, ameuawa kwa kuwakatakata mapanga wazazi wake na kisha kuchoma nyumba moto na kukimbia kusikojulikana.
Mauaji hayo yaliyotokea juzi saa 12:30 jioni yamesababisha simanzi kubwa katika kijiji hicho na kuwalazimu wananchi wa kijiji hicho kuanza kumsaka kijana huyo usiku kucha bila mafanikio.
Mwenyekiti wa kijiji cha Roo, Alfani Swai amethibitisha kutokea kwa mauaji hayo ambapo alisema mpaka sasa chanzo cha mauji hayo hakijafahamika na kuwataja waliopoteza maisha kuwa ni Shahidu Njau (60) na mkewe Minae Swai (57) .
Swai alisema wananchi waliamini nyumba imewaka moto kwa bahati mbaya lakini ghafla waliona mwili wa mwanamke ukiwa chini umetapakaa damu na umekatwakatwa kila mahali.
Alisema waliusogelea na kuugusa na kubaini tayari amefariki dunia na walipoangalia mbele waliona mwili wa mwanamume ukiwa umepasuliwa kichwa na ubongo uko nje huku akihema kwa shida ambapo walijitahidi kumwahisha hospitali na alipofika eneo la Sadala alipoteza maisha.

Mkuu wa wilaya ya Hai, Norvatus Makunga ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya hiyo alisema mpaka sasa sababu za kijana huyo kufanya mauaji makubwa kiasi hicho hazijajulikana .
Kamanda wa polisi mkoani hapa Robert Boaz amethibitisha kutokea kwa mauji hayo na kusema Jeshi la Polisi linaendelea kumsaka kijana huyo ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa.
SOURCE>>>MWANANCHI

No comments:

Post a Comment