Mwenyekiti wa Kamati namba tatu ya Bunge Maalumu la Katiba, Shamsi Vuai
Nahodha akiongoza mjadala wa kikao cha kamati hiyo mjini Dodoma jana.
Kulia ni mjumbe wa kamati hiyo, Anne Makinda. Picha na BMK
Dodoma. Bunge la Katiba jana
lilianza kujadili Rasimu ya Katiba kwa misukosuko kwenye Kamati baada ya
kuvamiwa na kundi la wanaharakati waliokuwa na mabango wakidai hati
halisi ya Muungano yenye saini za Mwalimu Julius Nyerere na Abeid
Karume.
Msukosuko mwingine uliozikumba karibu kamati zote
zinazoanza kujadili rasimu hiyo kwa kuanzia sura mbili zinazohusu
Muungano – sura ya kwanza na ya sita na kuzua malumbano, ni maana ya
maneno dola, shirikisho, muungano na nchi.
Wakati waandamanaji wenye mabango wakiishia
mikononi mwa polisi, suala la Muungano lilitulizwa kwa kuitwa wanasheria
kutoa tafsiri sahihi kwa kila neno.
Katika kamati zote, suala la muda wa kamati
kujadili sura hizo mbili kwa siku mbili kila moja pia liliibua mjadala
mkali, hadi kuwalazimisha baadhi ya wenyeviti wa kamati kuamua
kumwandikia mwenyekiti wa Bunge, Samuel Sitta kuomba muda uongezwe.
Hali hiyo imejitokeza Bunge hilo likiwa limeshakaa
siku 40 kabla ya kuingia katika mjadala rasmi, baada ya kupoteza muda
mwingi katika kutengeneza kanuni za uendeshaji wa chombo hicho.
Wanaharakati wavamia
Wakati kamati zikijiandaa kuanza mjadala,
wanaharakati wawili walivamia kwenye ukumbi wa Royal Village, wakiwa na
mabango yenye maandishi yanayowataka wajumbe kutetea maoni ya wananchi
yaliyomo kwenye rasimu ya Katiba.
Hata hivyo, watu hao baadaye waliondolewa kwenye eneo la hoteli hiyo na maofisa wa
usalama majira ya saa 2:00 asubuhi.
usalama majira ya saa 2:00 asubuhi.
Hata hivyo, mwenyekiti wa Kamati Namba 9, ambayo
inafanya vikao vyake kwenye hoteli hiyo, Kidawa Hamis alisema kuwa hali
ni shwari kwenye kamati yake na wajumbe wanaendelea kuchambua rasimu.
Katika kumbi zilizopo kwenye Hoteli ya St. Gasper,
pia watu wawili walikamatwa wakiwa na mabango yanayowataka wajumbe
kutambua kwamba katiba ni mali ya wananchi na si ya wanasiasa.
Hati ya Muungano
Katika makundi karibu yote, jana kuliibuka hoja
juu ya Hati ya Muungano, wajumbe wakitaka kabla ya kuanza mjadala
ionyeshwe kwa kuwa ndio msingi wa hoja.
No comments:
Post a Comment