Mjumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, Felix Mkosamali.PICHA|FILE
Dodoma. Mjumbe wa Bunge Maalumu
la Katiba, Felix Mkosamali (pichani chini), jana alirusha tuhuma kwa
Rais Jakaya Kikwete na Spika wa Bunge Muungano, Anne Makinda akidai kuwa
ni viongozi vigeugeu kutokana na kutaka mfumo wa serikali mbili.
Kutokana na hilo, Mkosamali alipendekeza wajumbe
wote wanaopinga mfumo wa serikali tatu, wabebe mabegi yao na kuondoka
bungeni kwa kuwa hawako tayari kuona katiba inatungwa ya CCM pekee.
Alitoa kauli hiyo alipokuwa akitoa mchango wake
kwenye Rasimu ya Katiba katika Sura ya Kwanza na Sura ya Sita ambayo
wajumbe walianza kuchangia jana.
Hata hivyo, Mwenyekiti wa Bunge, Samuel Sitta
alimtaka mjumbe huyo kufuta kauli yake ya viongozi vigeugeu ili
kupunguza kelele za wajumbe ambao walianza kuzomea kuwa alikuwa anakiuka
kanuni.
Mkosamali ambaye ni Mbunge wa Kibondo
(NCCR-Mageuzi), alisema kuwa nchi ya Tanzania haitasonga mbele kutokana
na kuongozwa na watu ambao ni vigeugeu.
Aliwatuhumu viongozi hao kuwa wamekuwa wakitenga
fedha nyingi kwa ajili ya kufanya propaganda za kulipana posho huku
wakilitupa na kulisahau Azimio la Arusha ambalo lilikuwa na maadili
mema.
Alisema wanachokifanya wajumbe wa CCM ni kupuuza
maoni ya Tume ya Jaji Joseph Warioba ili waendelee kutengeneza Katiba ya
kukaa mahali na kulipana rushwa.
“Mnajifungia ndani watu wawili mnaandika maoni
yenu kisha mnaleta yanakuwa ni maoni ya kukariri, mnapopuuza maoni ya
wananchi kwa serikali tatu, hizo mbili mlipata maoni ya watu gani?”
alisema.
Mapema jana Asha Bakari Makame, nusura achafue
hali ya hewa bungeni wakati akichangia kwenye rasimu hiyo baada ya
kuanza kumshambulia Ismail Jussa kwamba analazimisha muundo wa serikali
tatu ambao hautawezekana.SOURCE>>>>>MWANANCHI
No comments:
Post a Comment