NA:
MSHAMU NGONJWIKE……….Dr es salaam
TIMU 20 zinatarajiwa
kushiriki mashindano ya Kung Fu ya Kichina yatakayofanyika kuanzia
Juni 6 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na SWACOTZ FORUM jijini Dar es
Salaam, Mwenyekiti wa Taifa wa mchezo huo Mwarani Mutee alisema
mashindano hayo yatawahusu wanachama wao ambao ni hai ambao ndi watakaoruhusiwa
kushiriki.
“Tunategemea kufanya
mashindano makubwa Juni 6 Dar es Salaa, timu 20 zinatarajiwa kushiriki
katika mashindani hayo.
“Watakaoruhusiwa
kushiriki mashindano hayo ni wale wanachama ambao ni hai wanaofuata taratibu na
kanuni zetu,” alisema.
Alisema lengo la
mashindano hayo ni kuhakikisha mchezo huo unakuwa maarufu kwa wapenda kama
ilivyo michezo mingine, kudumisha undugu na kuwaleta watu pamoja.
“Lengo kubwa ni
kuhakikisha mchezo wetu unakuwa maarufu kama ilivyo michezo mingine, pia
kuwaleta wanamichezo pamoja na kubadilishana mawazo,” alisema.
No comments:
Post a Comment