NA MSHAMU NGOJWIKE……..Dar
es salaam
TIMU ya mpira wa
Magongo ya Magereza Ukonga inatarajiwa kushuka dimbani Jumapili wiki hii
kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya timu ya Dar es Salaam Institute (DI) ikiwa
ni moja wa maandalizi yao ya mashindano ya klabu bingwa ya Muunguano.
Akizungumza na SWACOTZ FORUM jijini Dar es Salaam
jana, kocha mkuu wa timu hiyo Merika Kahola alisema kuwa mechi hiyo itakuwa ya
kwanza katika orodha yao ya mechi za kirafiki kabla ya kuanza michuano hiyo.
Alisema kuwa mchezo
huo utakuwa ni moja ya kipimo kwa kikosi chake kinachojiandaa na michuano ya klabu
bingwa ya Muungano inayotarajiwa kuanza Machi 14 hadi 17 mwaka huu jijini Dar
es Salaam.
Kahola alisema kuwa
baada ya mechi hiyo timu yake itakuwa na mechi nyingine ya kujipima nguvu dhidi
ya timu ya Dar Kalsa ambayo watapanga ni lini watacheza mechi hiyo.
“Tumeshafanya
maandalizi ya kutosha kwa ajili ya michuano ya klabu Bingwa ya Muungano, hiyo
kwa sasa tutacheza mechi kadhaa za kirafiki kabla ya kuingia kwenye michuano
hiyo rasmi ambapo kwa kuanzia Jumapili tutacheza na Dar es Salaam Institute kwenye
Uwanja wetu wa magereza” alisema.
Alisema kuwa baada ya
kutwaa ubingwa wa kombe la miaka 50 ya mapinduzi ya Zanzibar sasa anakiandaa
kikosi chake kwa ajili ya kufanya vizuri kwenye mashindano hayo.
No comments:
Post a Comment