![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhWU9VbbDhRH-ZmqiL9Rx2lYi89VyRCYAwAPzmdvmEpNPBJIjE_XIZQRNMoSsQAOJpogOttweor91r7av_zy8gfSAXfFVreAsq1-da1LlAJl_vCdA1PolRAA1OEoNbXNmA1IMMGsuMe2FE/s1600/4.jpg) |
WALIMU AMBAO NI WANACHAMA WA cwt WAKIWA KATIKA KIKAO CHA UFUNGUZI WA BANK YAO LEO ASUBUHI |
NA: MOHAMED MWAYA........Mtwara
Chama cha walimu mkoa wa mtwara kimefanikiwa kufungua bank ambayo itakuwa ikihudumia jamii pamoja na wanachama wake kwa masuala mbalimbali ya kifedha kama sehem ya kuhakikisha chama hicho kinaweza kujimudu na kuendesha mambo yake ili kuwezesha elimu ya tanzania kuinuka toka pale tulipo sasa na kufika katika hali mzuri ya kiwango cha elimu nchini.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhOEj2s_FqmAGESAJ_HgoJ93WDalRyywfnpUZp7BJhRCHSJywuyL6yR5aMAT16VuMjBjKUR3anUTpbzeU0kJM0Zy4xJcnjDD89BdPxhc-lWmohVcaRa6EXace5j6GMFr2qUL_Abv4Wrbfg/s1600/3.jpg) |
AFISA UTUMISHI MANISPAA YA MTWARA MIKINDANI NDG:BARAKA KILAGU AKIONGEA NA WALIMU KWA NIABA YA MKURUGENZI (Picha na bakari chijumba) |
katika ufunguzi na utambulishi wa bank hiyo unaoendelea hivi sasa katika ukumbi wa chama hicho mkoani mtwara uliopo katika eneo la bima mtwara mjini jirani na ofisi za shirika la postaaliyekuwa mgeni rasmi kwa niaba ya mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya manispaa ya Mtwara Mikindani ambaye ni Afisa Utumishi wa manispaa ndg: Baraka Kilagu amesema kwa niaba ya mkurugenzi na ofisi ya manispaa ya mtwara mikindani wanakipongeza chama hicho cha walimu mkoa wa mtwara kwa hatua kubwa waliyoifikia ya kuamua kuwa na bank hiyo ya walimu ambayo itafahamika kama MCBL. MWALIMU COMMUSION BANK LIMITED kwakua vyama vingi vya mikoa mbalimbali vimeshindwa kufikia hatua kama hiyo."Ninawapomgeza sana kwa niaba ya mkurugenzi na ofisi ya manispaa sisi kama serikali tumepokea kwa moyo mmoja uamuzi wenu na tunaahidi kuwaunga mkono kwani ni hatua kubwa na muhimu ambayo vyama vingi vimeshindwa kuifikia" alisema Baraka Kilagu mapema leo asubuhi ndani ya ukumbi wa chama cha walimu tanzania tawi la mtwara wakati akizungumza na waalimu na uongozi wa chama hicho katika hafla ya utambulisho na ufunguzi wa bank hiyo.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEinA4cCmiWEOlq6HeyYPTO_9BdMYISBS0l7MAqe8NLi1Fa-cAS-Tdf_F4zaTP93X0Lm2LOWyrd4V2GSnrfGi5kKQTD2vdT-vhcPm_zuaaC_xJ2P4VWlRa2JQ1Fvtqk7XFVROnwtbM3CdT8/s1600/7.jpg) |
KATIBU WA CWT MKOA ...NDG:MATAMILA ACHIKUO (Picha na bakari chijumba) |
Kwa upande wake kaimu afisa elimu msingi Manispaa Bi: Cartheline Nguli amekiomba chama cha walimu na idara zake zote za elimu kujenga mahusiano yaliyotukuka ili kuhakikisha elimu inapanda mkoani mtwara.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhIUM-2jy_-iIMV2COkbrPLyOwE4-myxkIOJbryaPIp6uADGbXAYUk2tygWZ4crWJ5r_iM-mjWSF8nT5KI_rexSI09TuPreGEDYHORrx4vlhUGAeweD2JPPBSBIqSAzmuybBq2NNFstYp4/s1600/5.jpg) |
(Picha na bakari chijumba) |
Bank hiyo kwa sasa itaanza kwa kufungua matawi yake katika mikoa minne ambayo ni MBEYA,ARUSHA,DAR ES SALAAM NA MTWARA.
No comments:
Post a Comment