EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Thursday, March 6, 2014

SBL YAMPELEKA MSHINDI WAKE BRAZIL

NA MWANDISHI WETU
KAMPUNI ya Bia ya Serengeti (SBL) inatarajia wiki hii kupata mshindi wake wa kwanza wa safari ya Brazil katika droo yake ya nne ya Winda safari ya Brazil na Serengeti.
Hadi sasa washindi mbalimbali wamejishindia zawadi  ikiwemo ving’amuzi, ipad, bia za bure, na fedha taslimu.
Mshindi huyo wa safari ya Brazil atalipiwa gharama zote ambapo atatembelea vivutio mbalimbali nchini humo.
Meneja wa Bia ya Serengeti Rodney Rugambo alisema juzi jijini Dar es Salaam kuwa mpaka sasa washindi watano wamejishindia simu aina ya Samsung Galaxy Tab na wengine 18 wameshinda
ving’amuzi kupitia promosheni hiyo.
“Tunapenda kuwaambia wateja wetu kuwa wiki hii kutakuwa na droo kubwa yakupata mshindi wa kwanza wa safari ya Brazili ambaye atalipiwa gharama zote na Kampuni ya Bia ya Serengeti.
“Zawadi hii kubwa ni kwa ajili ya wateja wetu na cha kufanya ili kushinda zawadi na safari hiyo ni kufungua bia yako ya Serengeti kokote nchini na kufuatilia maelezo ya promosheni na unaweza kuwa mshindi wetu wa wiki inayokuja,” alisema.
Mmoja wa washindi wa simu ya Samsung Tab, Vedastus Kalinga kutoka Mbeya, aliishukuru SBL na kusema amefarijika kupata zawadi hiyo itakayomsaidia kufanya vitu vyake kwa urahisi zaidi katika ulimwengu huu wa dijitali licha ya kuwa ndoto yake ni kupata safari ya kwenda Brazil.

No comments:

Post a Comment