NA msham ngojwika ...dAR ES SALAAM
BONDIA Bernard Mwakasanga 'Shoka ya Bucha ' ameingia kambini
kwa ajili ya kujiandaa na mpambano lisilokuwa la ubingwa uzito wa juu dhidi ya
Iddi Kipandu utakaofanyika wa March 23 mwaka huu kwenye Ukumbi wa Friends Corner
Manzese, Dar es salaam.
Mpambano huo ambao unasubiliwa kwa hamu kubwa na mashabiki
wa masumbwi, homa yake imezidi kupamba moto baada ya kila mmoja kumtambia
mwenzake kuwa atammaliza raundi za awali.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana Mwakasanga alisema
Bonge ni kama nyama ya bucha hivyo ajiandae kumuondoa kwenye raundi ya kwanwa
ya mpambano huo.
Mratibu wa mpambano huo Waziri Rosta alisem kuwa mpambano huo
utakuwa na mapambano mengine kadhaa ya utangulizi ambapo bondia Fadhili Mjia 'Stoper'
ataonyeshana ubabe na Juma Selemani huku Twalibu Mchanjo akikutana na Mohamed
Babeshi.
Wengine ni Hassani Mandula akipambana na Ally Bugingo
mpambano mwingine utawakutanisha Amani Bariki na Selemani Motto, Halidi Manjee
akioneshana umwamba na Shabani Mtengela huku Mustafa Dotto akizichapa na Ismail
Ndende na Salimu Chagogo atapigana na Salumu Kombe.
Rosta alisema kuwa ulinzi na usalama utakuwa wa kutosha katika mpambano huo ili kuwapa fursa majaji kutoa maamuzi ya haki na usawa.
Rosta alisema kuwa ulinzi na usalama utakuwa wa kutosha katika mpambano huo ili kuwapa fursa majaji kutoa maamuzi ya haki na usawa.
No comments:
Post a Comment