Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki, Papa Francis.PICHA|MAKTABA
Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki, Papa Francis ametimiza mwaka mmoja tangu alipochaguliwa kushika wadhifa huo.
Katika miezi yake 12 ya uongozi, Papa Francis
amefanya mambo kadhaa muhimu ambayo watangulizi wake walishindwa
kuyafanya, huku akitoa kipaumbele katika ujenzi wa kanisa hilo katika
maeneo yenye ongezeko kubwa la watu na kuwajali masikini.
Papa Francis aliingia madarakani Machi 13, 2013 na
kupewa nafasi ya kuliongoza kanisa hilo lenye zaidi ya waumini bilioni
1.2 duniani.
Miongoni mwa mambo yasiyo ya kawaida aliyofanya baada ya kuchaguliwa, ni pamoja na kukataa kutumia gari maalumu kwa ajili yake.
Gari hilo lilikuwa limefunikwa kwa kioo, hivyo
kukiuka utaratibu wa awali uliowekwa na Kanisa wa kuwalinda viongozi wao
wakuu baada ya Papa John Paul II kupigwa risasi.
Pia Papa Francis aliwahi kusafiri katika basi moja
na makadinali. Kama haitoshi, pia alikataa kutumia gari aina ya
Mercedes, badala yake alitumia gari aina ya Renault iliyokuwa na miaka
20, huku ikiwa imetembea
zaidi ya kilomita laki mbili.
zaidi ya kilomita laki mbili.
Akielezea aina ya uongozi wake, mwandishi Chris
Boeskool anasema uamuzi huo siyo tu ni wa hatari kwa usalama, bali
unaonyesha ni namna gani asivyojali kuhusu kifo.
Pia, Papa Francis anaamini kuwa kufanya jambo zuri ni bora kuliko kuamini jambo hilo na kuishia kulisema tu.
“Bwana ametukomboa sisi sote, siyo Wakatoliki peke yao wanaoamini kuwapo kwa Mungu na wasioamini,” aliwahi kusema.
Pamoja na umri wake mkubwa, Papa Francis amekuwa
mtumiaji mzuri wa mitandao ya kijamii. Kwa mfano, akaunti yake ya
mtandao wa Twitter ina watu zaidi ya milioni tatu wanaomfuatilia duniani
kote.
>>>MWANANCHI
>>>MWANANCHI
No comments:
Post a Comment