EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Monday, February 24, 2014

WALINZI WA MAKAMPUNI MTWARA WAILILIA SERIKALI




Reporters/ Mohamedi & Aloyce
 Wafanyakazi wa makampuni mbalimbali ya ulinzi Mkoani Mtwara wameuomba uongozi wa makampuni hayo kuwaongezea mishahara na kulipwa malipo yao kwa wakati.

Hayo yamezungumzwa mapema hii leo na baadhi ya wafanyakazi hao wakati walipokuwa wanazungumza na waandishi wa habari wa Prde Fm Radio.
Wafanyakazi hao ambao hawakupenda majina yao yatajwe wamesema kuwa hawalipwi malipo yao kwa wakati na vilevile kuwepo kwa vitendo vya unyanyasaji hali inayopelekea maisha yao kuwa magumu.
Pia wafanyakazi hao wameuomba uongozi wa makampuni hayo kushughulikia matatizo yao likiwemo la kutopewa likizo ilikuepukana na matatizo ambayo wamekuwa wakiyapata.

No comments:

Post a Comment