Mornitoring/ Mdenga.
Reporters/ Mohamedi & Aloyce.
Wakazi waishio katika mtaaa wa Mdenga Mkoani Mtwara
waiomba serikali kuhamisha au koboresha mazingira ya dampo la kuchomea sumu la
SBS ili kuepukana na adha ambazo wamekuwa wakizipata kutokana na uwepo wa dampo
hilo.
Hayo yamezumgumzwa mapema hii leo na wakazi hao
wakati wakizungumza na waandishi wa habari wa Pride Fm Radio katika eneo hilo.
Mmoja wa wakazi hao Ayubu Rashidi amesema wamekuwa
wakipata adha mbalimbali kutokana na uwepo wa dampo hilo ikiwemo ya harufu kali
na maradhi ya kifua yanayotokana na moshi wenye kemikali za sumu.
Pia Subira Ndege ni mmoja wa wakazi waishio eneo
hilo amesema kuwa kutokana na dampo hilo kutililisha maji machafu yenye sumu
katika dimwi la maji ambayo wamekuwa wakiyatumia katika maisha yao ya kila siku
wamekuwa wakipata matatizo mbalimbali yakiwemo ya kuwashwa mwili pindi
watumiapo maji hayo.
No comments:
Post a Comment