EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Saturday, February 15, 2014

Muumini awapania Choki, Banza

NA MSHAMU NGOJWIKE,Dar



MUIMBAJI mahiri wa muziki wa dansi Nchini Muumini Mwinjuma ‘Kocha wa Dunia’ amejipanga kuwafunika nguli wenzake Ally Choki na Ramadhani Masanja ‘Banza stone’ katika uzinduzi wa albamu ya Mtenda akitendewa ya bendi ya Extra bongo utakaofanyika Februari 22 katika ukumbi wa Dar live, Mbagala.

 mwinjuma muumin

Uzinduzi huo unaenda sambamba na albamu ya Mkurugenzi wa bendi hiyo Ally Choki iliyo katika mtindo wa Rhumba akiwa amewashirikisha wanamuziki mbalimbali nchini wa dansi, Bongo fleva, Hip hop na Taarabu.
Akizungumza na DIMBA jana, Muumini alisema anawaonea huruma sana wanamuziki hao kwani ni lazima atawafunika katika uzinduzi huo na watajuta kumualika.

 mwinjuma ndani ya kazi

“Nimealikwa kusindikiza tu lakini watajutia uamuzi wao huo kwani ni lazima ni wafunike nadhani wote wananijua uwezo wangu na huwa sifanyi makosa katika shoo kama hizi hivyo wajiandae kuwa nyuma yangu,” alisema.
 banza stone atakinukisha dar live

 banza na Alliy Choki wote watakinukisha Dar live
Aliongeza kuwa baada ya kufanya makubwa katika uzinduzi huo ndipo ataelekeza nguvu katika kutangaza wanamuziki wake wapya  atakaokuwa nao katika bendi yake huko itakayokuwa na maskani yake mjini Kahama.

No comments:

Post a Comment