NA : KASSIM NGUMBI
Mkuu Wa
Wilaya Ya Mtwara Ameanza Shughuli Ya Ugawaji Wa Mahindi Ya Msaada Kwa Kata
Mbalimbali Za Halmashauri Ya Mtwara Vijijini Ili Kukinga Hali Mbaya Inayowza
Kujitokeza Wakati Wowote Ya Wananchi Kukosa Chakula Kutokana Na Hali Ya Hewa
Kutokuwa Mzuri Na Kupelekea Baadhi Ya Mzao Yaliyoko Mashambani Kama Vile
Mahindi Kuanza Kukauka Huku Ayakiwa
Tayari Yalifikia Katika Hatua Ya Kukarbia Kuliwa Nah Ii Inatokana Na Hali Ya
Kutokuwepo Kwa Mvua Ndani Ya Msimu Huu
Wa Masika Mkoani Mtwara.
SWACOTZ
FORUM Ilishuhudia Hali Ya Mashamba Mbalimbali Ilivyo Huko Vijijini Wakati
Ilipotembelea Maeneo Mbalimbali Ya Mtwara Vijijini Mwishoni Mwa Wiki Iliyopita
Kaa Vile Eneo La Kivava Boda Ambako Ni Mpakani Mwa Tanzania Na Msumbiji Pamoja
Na Kitaya,Mahurunga Na Kitere N Kushuhudia Hali Ya Mahindi Yaliyokauka Na Mazao
Mengine Lakini Pia Mwandishi Wa
Mkuu Wa Wilaya Ya Mtwara Ameanza Shughuli Ya Ugawaji Wa Mahindi Ya Msaada Kwa Kata Mbalimbali Za Halmashauri Ya Mtwara Vijijini Ili Kukinga Hali Mbaya Inayowza Kujitokeza Wakati Wowote Ya Wananchi Kukosa Chakula Kutokana Na Hali Ya Hewa Kutokuwa Mzuri Na Kupelekea Baadhi Ya Mzao Yaliyoko Mashambani Kama Vile Mahindi Kuanza Kukauka Huku Ayakiwa Tayari Yalifikia Katika Hatua Ya Kukarbia Kuliwa Nah Ii Inatokana Na Hali Ya Kutokuwepo Kwa Mvua Ndani Ya Msimu Huu Wa Masika Mkoani Mtwara.
Habari Hii Alipofika Katika Kata Ya Njengwa
Wananchi Walimweleza Hali Halisi Iliyoko Katika Maeneo Hayo Ambapo Kwakweli Hali
Ni Mbaya Ambapo Moja Ya Wananchi Hao Aliyejitambulisha Kwa Jina Moja La Rehema
Salum Ambaye Pia Ni Mzazi Wa Watoto Watatu Alisema Kuwa Katika Hali Isiyo Ya
Kawaida Na Haijawahi Tikea Mwaka Huu Imeonekana Kuuuandama Mkoa Wa Mtwara Kwa
Mazao Kukauka Kutokana Na Jua Kali Linaloendelea Kuwaka Kila Siku Zinaposogea
Baadhi Ya Sehem Mazao Yalionekana Kuja Vizuri Na Kufikia Hatua Ya Kuleta
Tumaini La Kuliwa Kwa Mfano Mahindi Tayari Yameanza Kuchanua Na Mengine Kubeba
Magunzi Lakini Jua Limeanza Kuwaka Mfululizo Na Kupelekea Mazao Hayo Kuanza
Kukauka Huku Wananchi Wakiwa Hwana Chakula Na Hawajuwi Nini Cha Kufanya Aidha
Mwanamke Huyo Alisema Kuwa Wao Katika Kijiji Chao Cha Chihwindi Kilichopo Kata
Ya Njengwa Almashauri Ya Mtwara Vijijini Mkoani Mtwara Tayari Wameanza Mikakati
Ya Kuangalia Uwezekano Wa Kuifunga Shule Ya Msingi Iliyoko Katika Eneo Lao
Kutokana Na Haloi Kuzidi Kuwa Mbaya Kwani Watoto Wamekuwa Wakishindwa Kusoma
Kutokana Na Njaa Na Badala Yake Wengi Wanaishia Vichakani Kuchuma Matunda Poli
Na Kuyala Wakati Ambao Walitakiwa Kwenda Shuleni, Pia Alieleza Kuwa Hali Hiyo
Inasababisah Hata Wananchi Wenyewe Kukata Tama Ya Kufanya Maandalizi Ya
Mashamba Mapya Kwa Ajili Ya Kilimo Cha Msimu Wa Kiangazi
“Tumeishiwa
Baba Hali Ni Mbaya We Si Unaona Mwenyewe Mahindi Yote Yamekauka Kwa Jua Hapa
Tunawaza Kuifunga Shule Ili Watoto Wakae Nymbani Sababu Ya Njaa” Alisema Mama
Huyo Akimuelezea Mwandishi Wa Habari Hizi Lakini Wakati Haya Yakiendelea
Serikali Ya Wilaya Ya Mtwara Kupitia Mkuu Wake Wa Wilaya MH: Wilman Kapenjama
Ndile Tayari Imeanza Kusambaza Mahindi Ya Msaada Kutokea Kwenye Mfuko Wa Maafa
Na Mahindi Hayo Yanasambazwa Kwenye Kila Kata Ili Kuzisaidia Kaya Za Maeneo
Husika Mara Baada Ya Kugundulika Kuwepo Kwa Hali Mbaya Ya Hewa Inayosababisha
Kupotea Kwa Mazao Yaliyoko Mashambani.Mahindi Hayo Yatakuwa Yakiuzwa Shilingi
50 Kwa Kilo Mojha Na Kila Kaya Itapata Kulingana Na Mpangilio Uliopangwa. Lakini baadhi ya viongozi tayari wameanza
kuzungumza na makundi mbalimbali ya wananchi na kuwashauri kulima vilimo
mbadala kama vile ufuta na huku muhogo ukipewa kipaumbele na kuonekana kuwa ni
kilimo pekee kitakachoikomboa mtwara kwa mwaka huu kutokana na kuvumilia hali
ya ukame.
MBUNGE WA CHADEMA AFIKISHWA MAHAKAMANI
Mbunge wa Jimbo la Maswa Mashariki (Chadema), Sylvester Kasulumbayi.PICHA|MAKTABA
Na Shija Felician, Mwananchi
Kahama. Mbunge wa Jimbo la
Maswa Mashariki (Chadema), Sylvester Kasulumbayi na Diwani wa Kata ya
Buselesele, Crispian Kagoma na watu wengine 14 wamepandishwa kizimbani
kwa tuhuma za kujeruhi katika vurugu zilizoibuka katika kampeni za
uchaguzi mdogo wa udiwani wilayani Kahama mkoani Shinyanga.
Kasulumbayi na wenzake 15, ambao wanaaminika kuwa
wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) walifikishwa
katika Mahakama ya Wilaya ya Kahama saa 8.00 mchana jana na kusomewa
mashtaka sita kila mmoja.
Akisoma mashtaka hayo mbele ya Hakimu Mfawidhi
Mwandamizi wa Mahakama ya Wilaya ya Kahama, Gadiel Mariki, Mwendesha
Mashtaka Shukrani Madulu alisema washtakiwa wote kwa pamoja walitenda
makosa hayo Februari 4, mwaka huu.
Madulu aliiambia mahakama hiyo kuwa washtakiwa hao
wakiongozwa na mbunge huyo walitenda kosa hilo la kuwashambulia kwa
mapanga wafuasi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakati wa kampeni za
kuwania udiwani wa Kata ya Ubagwe katika Halmashauri ya Wilaya ya
Ushetu.
Alisema mashtaka matano ni kushambulia na kujeruhi
kwa mapanga, na moja la kuharibu mali, ikidaiwa kuwa katika vurugu hizo
washtakiwa waliishambulia gari la CCM la wilaya hiyo na kuliharibu.
Washtakiwa wote walikana mashtaka yote na kuomba
mahakama iwape dhamana ili waendelee na kampeni za kumnadi mgombea wao
wa nafasi ya udiwani katika kata hiyo ya Ubagwe.
Maombi hayo yalipingwa na Mwendesha Mashtaka,
akiiomba mahakama isitoe dhamana kwa kuwa hali za majeruhi watatu ni
mbaya kwa kuwa tayari wamepelekwa kwenye Hospitali ya Rufaa na Bugando
mkoani Mwanza, baada ya matibabu yao kushindikana wilayani Kahama.
Kutokana na hali hiyo, Hakimu Mariki alikubaliana na hoja hiyo na kuahirisha kesi hiyo hadi leo ambapo kesi hiyo itasikilizwa.
Watuhumiwa wote walipelekwa mahabusu baada ya dhamana hiyo kuzuiliwa.
Waliojeruhiwa kwenye vurugu
Wafuasi watano wa CCM wilayani Kahama akiwamo ofisa mtendaji wa Kata ya Ubagwe walijeruhiwa kwa mapanga kwenye vurugu hizo.
Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Andrew Emmanuel
alisema Masunga, Kamaro na Peter walisafirishwa kwenda Bugando jijini
Mwanza kwa matibabu zaidi.
No comments:
Post a Comment