Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuzindua rasmi Mtambo wa Kuhakiki Takwimu za Mawasiliano (Telecommunication Traffic Monitoring System) leo February 27, 2014 katika jengo la Mawasiliano Towers jijini Dar es salaam. Kulia ni Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Pro, Makame Mnyaa Mbarawa, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Prof. John Nkoma, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Saidi Meck Sadick na wadau wengine wa tehama.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akibofya kitufe kuzindua rasmi Mtambo wa Kuhakiki Takwimu za Mawasiliano (Telecommunication Traffic Monitoring System) leo February 27, 2014 katika jengo la Mawasiliano Towers jijini Dar es salaam.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo ya Mtambo wa Kuhakiki Takwimu za
Mawasiliano (Telecommunication Traffic Monitoring System) aliouzindua
leo February 27, 2014 katika jengo la Mawasiliano Towers jijini Dar es
salaam. Kulia ni Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Pro, Makame Mnyaa Mbarawa, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Prof. John Nkoma, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Saidi Meck Sadick na wadau wengine wa tehama.
Rais
Jakaya Kikwete ameiagiza Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
kuhakikisha mchakato wa Sheria ya Usalama kwenye mitandao unakamilika
na kuanza kutumika, ili kudhibiti wanaotoa siri za nchi kwa kisingizio
cha uhuru wa habari.
Hayo aliyasema jana kwenye hafla ya uzinduzi wa
mtambo maalumu wa usimamizi na uhakiki wa Mawasiliano ya Simu, (TTMS),
iliyofanyika Ofisi za Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA) Dar es
Salaam.
Rais Kikwete alisema hakuna nchi yoyote duniani
ambayo haitunzi siri zake, kwa kuwa jambo hilo ni muhimu kiusalama, hata
kwa mataifa ambayo yamekuwa mstari wa mbele kutetea uhuru wa vyombo vya
habari.
Alisisitiza kwa kumtolea mfano aliyekuwa Jasusi wa
Marekani, Edward Snowden, anatuhumiwa kuvujisha siri za nchi hiyo
kwenye mtandao, ambaye sasa amekimbilia mafichoni Urusi. Aliwapongeza
TCRA kwa hatua hiyo, akieleza kuwa inawezesha uchumi wa nchi kupata
kichocheo cha kukua kwa kuwa sasa kutakuwa na udhibiti wa mawasiliano
hasa ya simu za nje ya nchi na kuongeza kipato kwa taifa.
Awali Mkurugenzi wa TCRA, Profesa John Nkoma
alisema kufungwa kwa mitambo hiyo, kunakwenda pamoja na kuwapo kwa
kanuni mpya za mawasiliano ya usimamizi na uhakiki wa mawasiliano ya
simu (TTMS, Regulation 2013), ambapo imewezesha Serikali kupata senti 7
kati ya 25 zinazotozwa kwa kila dakika na nyingine zinagawanywa kwa
kampuni husika.
“TCRA imefanikiwa kuilipa Hazina mgawo wa mwezi
Oktoba, kwa mujibu wa Sheria ya TMMS Sh1.6 bilioni, leo tutakabidhi
malipo ya Sh1.6 bilioni malipo ya Novemba hatimaye mwezi Machi tutalipa
ya Desemba,” alisema Nkoma.
No comments:
Post a Comment