EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Saturday, February 15, 2014

CCM YAWATIA KIKAANGONI MAKAMBA NA WASIRA


Waziri wa Nchi ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu) Stephen Wassira akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuhojiwa na kamati ya maadili ya CCM mjini Dodoma . na Mpigapicha wetu 

Posted  Februari15  2014  saa 9:0 AM

Dodoma. Kamati ndogo ya Maadili ya CCM imeendelea kuwahoji wanachama wake walioonyesha nia ya kuwania urais, jana ilikuwa zamu ya mawaziri watatu.
Waliohojiwa jana ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mahusiano na Uratibu, Stephen Wassira na Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Januari Makamba. Makamba alikuwa wa kwanza kufika mbele ya kamati hiyo jana asubuhi, huku Wassira akifuatia. Hata hivyo, Membe hakuonekana.
Hata hivyo, kanuni za uongozi wa maadili za CCM kifungu cha 7 (i) kinaeleza kuwa wanachama wenye nia ya kugombea nafasi za uongozi katika muhula unaofuata, yaani ubunge, uwakilishi, udiwani na nafasi nyingine katika chama wanaweza kutangaza nia zao, lakini hawaruhusiwi kufanya kampeni kabla ya muda uliowekwa rasmi, muda wa kampeni unaanza baada ya majina ya wagombea kuteuliwa na kikao kinachohusika.

Makamba
Baada ya kuhojiwa Makamba, alisema siyo vibaya kwa wanaotaka kuwania urais katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 kutangaza nia mapema, kwa sababu inawapa nafasi wananchi kuwapima.
Mbali na hilo Makamba alisema siyo dhambi kwa mtu kuonyesha nia, bali ni dhambi kwa mtu kutoa fedha kwa nia ya kutaka uongozi na kuvitaka vyombo vya dola kuchukua hatua za kisheria kwa watu wa aina hiyo.
Kikao hicho kinachoongozwa na Makamu Mwenyekiti Bara, Philip Mangula, juzi kiliwahoji mawaziri wakuu wa zamani Edward Lowassa na Fredrick Sumaye pamoja na Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja, ambaye pia aliwahi kuwa Waziri wa Nishati na Madini.
“Ipo faida ya kuwajua mapema wanaotaka uongozi kuliko kuwajua mwishoni, kwa sababu mnapata faida ya kuwachambua na kuwauliza maswali, mbaya ni mtu kutoa pesa ama kutumia pesa.
“Hata katika maoni yangu na ushauri (ndani ya kikao hicho cha maadili), nimesema kwamba hilo ndilo kubwa na la msingi, kwa sababu linawaweka pembeni watu wenye vipaji vya uongozi kama huna fedha basi huwezi kuwa kiongozi,” alisema Makamba.
Alisisitiza matumizi ya fedha katika kutafuta uongozi yanakatazwa kwa mujibu wa kanuni za chama chao na sheria za nchi na kwamba ushahidi unapopatikana chama kifanye kazi yake na Serikali ichukue hatua dhidi yao.
Makamba alisema ipo sheria ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na Sheria ya Gharama za Uchaguzi, ambazo zote zinakataza matumizi ya fedha.
“Kwa hiyo hawa wanaotajwa wanatumia fedha vilevile yombo vya dola viwachukulie hatua, siyo tu kwenye chama,” alisema Makamba.
>>>Mwananchi

No comments:

Post a Comment