EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Friday, February 28, 2014

ASHANT UNTED YAKUBALI KICHAPO CHA BAO 4-0 TOKA KWA AZAM

AZAM_FC_PLAYERSWakiwa kwao Azam Complex, Chamazi, kwenye Viunga vya Jiji la Dar es Salaam, Azam FC Jana waliichapa Ashanti United Bao 4-0 na kukaa kileleni mwa VPL, Ligi Kuu Vodacom.
Baada ya kucheza Mechi 18, Azam FC wako Nambari Wani wakiwa na Pointi 40 wakifuatiwa na Yanga waliocheza Mechi 17 na wana Pointi 38.
Bao za Azam Fc zilifungwa na Morris, kwa Penati, Said Morad na Gaudence Mwaikimba ambae alifunga Bao mbili.
Mwaikimba alikuwa kitambo hajaonekana Uwanjani na pengine amepata nafasi hii, ambayo aliitumia vyema kuonyesha makeke yake ya Siku za nyuma, kwa vile tu Mastraika wa kawaida wa Azam FC, kina Booco na Kipre Tchetche hawakuweza kucheza.
Tchetche anatumikia Adhabu ya kufungiwa Mechi baada kupata Kadi Nyekundu Mechi iliyopita waliyotoka Sare 2-2 na Tanzania Prisons.
Ligi hii itaendelea Jumapili kwa Mechi 5.

MSIMAMO:
NA TIMU P W D L GD PTS
1 Azam FC 18 11 7 0 23 40
2 Yanga SC 17 11 5 1 29 38
3 Mbeya City 19 9 8 2 8 35
4 Simba SC 19 8 8 3 16 32
5 Kagera Sugar 19 6 8 5 1 26
6 Coastal Union 19 5 10 4 5 25
7 Mtibwa Sugar 19 6 7 6 0 25
8 Ruvu Shooting 18 6 7 5 -4 25
9 JKT Ruvu 19 7 1 11 -13 22
10 Prisons FC 17 3 8 6 -3 17
11 Mgambo JKT 19 4 5 10 -17 17
12 JKT Oljoro 19 2 8 9 -15 14
13 Ashanti United 19 3 5 11 -19 14
14 Rhino Rangers 19 2 7 10 -11 13
RATIBA:
Jumapili Machi 2
Simba v Ruvu Shooting
Kagera Sugar v JKT Ruvu
Mbeya City v JKT Oljoro
Ashanti United v Rhino Rangers
Tanzania Prisons v Mgambo JKT

No comments:

Post a Comment