![]() |
KIUNGO REAL MADRID GALETH BALE AKIJARIBU KUIPITA NGOME YA SCHLAKE 04 |
VIGOGO wa Spain, Real Madrid, wapo mguu
mmoja ndani ya Robo Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI baada ya kuibonda
Schlake 04 Bao 6-1 huko Veltins Arena Jijini Gelsenkirchen Nchini
Germany katika Mechi ya Kwanza ya Raundi ya Mtoano Timu 16.
Wakicheza
Ugenini huko Veltins Arena Jijini Gelsenkirchen Nchini Germany, Real
Madrid walishinda Mechi hii ya Kwanza ya UEFA CHAMPIONZ LIGI, Raundi ya
Mtoano Timu 16, kwa kuichapa Schalke Bao 6-1 na hadi Mapumziko walikuwa
mbele kwa Bao 2-0.
Bao la kwanza lilifungwa Dakika ya 13
kwa kazi njema ya Gareth Bale aliempa Cristiano Ronaldo aliepiga kwa
kisigino na Mpira kuguswa na Beki Santana na kumfikia Karim Benzema
alieipa Real Bao.
Bao la Pili lilifungwa Dakika ya 21 na Gareth Bale baada ya kazi nzuri ya Benzema na Bale kufunga.
Katika Dakika ya 52, pasi ya Bale
ilimfikia Cristiano Ronaldo ambae alimhadaa Joel Matip na kisha kufunga
Goli kwa shuti la Mguu wa kushoto.
Dakika ya 57, Benzema akafunga Bao lake
la pili na la 4 kwa Real kufuatia pasi ya Ronaldo ya kisigino na katika
Dakika ya 69 Bale pia akafunga Bao lake la Pili na la 5 kwa Real baada
kupokea pasi ya Sergio Ramos.
Nae Ronaldo haukuachwa nyuma kwa kufunga
Bao 2 kwani katika Dakika ya 89 alipiga Bao baada Kiungo wa Schalke
Leon Goretzka kunyang'anywa Mpira na Isco aliempa Karim Benzema
aliempenyezea Cristiano Ronaldo na kuandika Bao la 6.
Schalke walifunga Bao lao pekee katika Dakika ya 90 Mfungaji akiwa Klaas-Jan Huntelaar.
VIKOSI:
Schalke: Fahrmann; Howedes, Matip, Felipe Santana, Kolasinac; Boateng, Neustadter; Farfan, Meyer, Draxler; Huntelaar
Akiba: Hildebrand, Hoogland, Goretzka, Papadopoulos, Obasi Ogbuke, Fuchs, Szalai.
Real Madrid: Casillas; Carvajal, Pepe, Sergio Ramos, Marcelo; Modric, Alonso, Di Maria; Bale, Benzema, Ronaldo
Akiba: Diego Lopez, Varane, Fabio Coentrao, Arbeloa, Jese, Isco, Illarramendi.
Refa: Howard Webb [England]
UEFA CHAMPIONZ LIGI
Raundi ya Mtoano ya Timu 16
MARUDIANO
[Kwenye Mabano Matokeo Mechi ya Kwanza]
[Saa za Bongo]
Jumanne Machi 11
22:45 Bayern Munich v Arsenal FC [2-0]
22:45 Atletico de Madrid v AC Milan [1-0]
Jumatano Machi 12
22:45 FC Barcelona v Manchester City [2-0]
22:45 Paris Saint-Germain v Bayer 04 Leverkusen [4-0]
Jumanne Machi 18
22:45 Chelsea FC v Galatasaray Spor Kulübü [1-1]
22:45 Real Madrid CF v Schalke 04 [1-6]
Jumatano Machi 19
22:45 BV Borussia Dortmund v Zenit St. Petersburg [4-2]
22:45 Manchester United v Olympiacos CFP [0-2]
No comments:
Post a Comment