EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Thursday, January 16, 2014

YANGA YAWAITA WANCHAMA KWA WINGI KWENYE MKUTANO WA JUMAPILI





.Uongozi wa Yanga umewataka wanachama wa klabu hiyo kujitokeza kwa wingi kwneye mkutano utakaofanyika Jumapili Januari 19 kwenye Ukumbi wa PTA Sabasaba jijini Dar es Salaam
Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga, amesema leo, mkutano huo utafanyika kuanzia Saa 3:00 asubuhi
.
.Sanga amewataka wanachama kujitokeza kwa wingi kwa kuwa hiyo ndiyo nafasi nzuri kwao kutoa na kufikisha mawazo yao kwa lengo la kusaidia ujenzi wa maendeleo klabu hiyo
Makamu huyo mwenyeki, alisema ndani ya mkutano huo  watajadili mambo kadhaa muhimu yanayohusiana na klabu yao ikiwa ni pamoja na kupanga mikakati madhubuti ya kutetea ubingwa.
Pamoja na hivyo, kwa pamoja wanachama hao watapanga mikakati imara ya kujiandaa na mashindano yenye malipo ya juu zaidi kwa ngazi ya klabu ya Ligi ya Mabingwa wa Afrika, hasa kama timu itafanikiwa kusonga mbele zaidi.

Awali Sanga alikuwa amezungumzia uamuzi wao wa kumpa Kocha, Hans van Der Pluijm, vyeo vitatu vya mkurugenzi wa ufundi, kocha mkuu na meneja.
Tayari kocha huyo raia wa Uholanzi yuko nchini Uturuki ambako ameungana na kikosi cha Yanga kilichoweka kambi nje kidogo ya mji wa Antalya.
SOURCE:MWANASPORT

No comments:

Post a Comment