Taarifa kutoka ndani ya Yanga zinaeleza,
uongozi wa klabu hiyo umepanga kumwaga kiasi cha Sh milioni 10 ili kuisaidia
michuano hiyo.
“Kweli Yanga ilishindwa kushiriki
michuano hiyo kutokana na kutokuwa na benchi la ufundi. Lakini heshima bado iko
juu na tunaiheshimu sana.
“Uongozi umeamua kuchangia gharama za
kuendesha michuano hiyo kwa kuwa tunajua umuhimu na heshima ya Yanga visiwani
Zanzibar.
“Pamoja na hivyo, siku tukiwa na nafasi,
basi timu itakwenda Zanzibar kucheza na kombaini ya huko kwa ajili ya kuonyesha
kuwa tunathamini,” kilieleza chanzo.
Uongozi wa juu wa Yanga ndiyo uliofikia
uamuzi huo ili kuonyesha kuwa haukuwa na nia ya kuidharau michuano hiyo.
Wakati ulipofika kwenda kwenye michuano
hiyo, Yanga ndiyo ilikuwa imetimua benchi lake lote la ufundi chini ya Kocha
Ernie Brandts, raia wa Uholanzi.
Sasa Yanga bado inahaha kusaka kocha
mkuu, huku msaidizi wake akiwa ni Charles Boniface Mkwasa ambaye anasaidia na
kocha wa makipa, Juma Pondamali.
Yanga inaondoka kesho alfajiri kwenda
nchini Uturuki ambako itaweka kambi katika mji wa Antalya.
Hii ni mara ya pili Yanga kuweka kambi katika mji huo wa kitalii nchini Uturuki.
SOURCE:SALEHE JEMBE
No comments:
Post a Comment