Mahakama ya Wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya, imewahukumu watu 29 kifungo cha miaka
mitatu jela kila mmoja ama kulipa faini ya Sh400,000 baada ya kutiwa hatiani
kwa makosa ya kuandamana bila kibali na kuvunja nyumba za ibada wakati wa
vurugu za kugombea kuchinja katika Mji wa Tunduma wilayani Momba mwaka jana.
Hakimu
Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Rahimu Mushi akisoma hukumu hiyo alisema mahakama
yake imeridhishwa na ushahidi uliotolewa na kwamba wanatiwa hatinani kwa
matendo yao.
Hata
hivyo ni washtakiwa watano tu kati yao waliokwenda jela, huku wengine 24
wakilipa faini.
Washtakiwa
hao walifikishwa mahakamani hapo Februari 4 mwaka jana, wakishtakiwa kwa makosa
sita ya kuandamana bila kibali, kufanya vurugu, kuharibu mali, kuchoma matairi
barabarani na kumpiga askari.
Mushi
alisema kulingana na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo, mahakama imeridhika
na kuwatia hatiani washitakiwa kwa makosa manne ya kuandamana bila kibali,
kuchoma matairi barabarani, kuvunja nyumba ya ibada nyumba ya askari na
kumjeruhi askari.
TUPE
MAONI YAKO
No comments:
Post a Comment