Ikulu imetaka kufungwa kwa mjadala wa kuhusu kurudishwa kwa mawaziri wanaodaiwa
kuwa ni mizigo kwenye Baraza la Mawaziri na badala imetaka waachwe wafanye
kazi.
Mkurugenzi
wa Mawasiliano Ikulu, Salva Rweyemamu alisema kuendeleza mjadala huo ni
kupoteza muda, kwani Rais Jakaya Kikwete alishamaliza kazi yake.
Rweyemamu
alisema Rais ndiye mwenye mamlaka ya kuteua mawaziri ambao wana wajibu wa
kumsaidia katika utekelezaji wa majukumu yake, hivyo si sahihi wateule hao
kuitwa ‘mizigo’ kwani yeye (Rais) ameona wanafaa.
“Rais
anapoteua watu anaangalia wanaofaa kumsaidia na si vinginevyo. Kwani lengo lake
ni kuona nchi ina `move forward’ (inasonga mbele) kimaendeleo,” alisema
Rweyemamu. Alisema watu wanapaswa kukumbuka kuwa mtu anapoteuliwa kwenye
uwaziri kuna suala la uwajibikaji: “Anatakiwa kutekeleza uwajibikaji wa pamoja.
Sasa kumshambulia mtu binafsi na kumwita mzigo siyo sahihi.”
Rweyemamu
alisema mjadala huo kwa sasa umepitwa na wakati na kuwataka wananchi na
wachambuzi kuwaacha mawaziri hao kuchapa kazi.
“Ni
vizuri wananchi wakawapa nafasi mawaziri hawa ya kufanya kazi na baadaye
kuwapima na kuwachambua kutokana na utendaji wao,” alisema.
Chimbuko
la majadala
Mjadala
kuhusu suala hilo unatokana na Rais Kikwete kuwarejesha katika Baraza la
Mawaziri baadhi ya mawaziri ambao walidaiwa kuwa ni mizigo kutokana na udhaifu
katika utendaji wao.
Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahaman Kinana na Katibu wake wa Itikadi na Uenezi, Nape
Nnauye ndiyo walioasisi mawaziri hao kuwa ni ‘mizigo’ walipokuwa na ziara ya
kikazi mkoani Ruvuma, mwishoni mwa mwaka jana.
Mawaziri
waliolalamikiwa kutokana na utendaji wao ni wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk
Shukuru Kawambwa, Kilimo, Chakula na Ushirika, Christopher Chiza, aliyekuwa
Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk David Mathayo, Waziri wa zamani wa
Fedha, marehemu Dk William Mgimwa na aliyekuwa Naibu wa Kilimo, Chakula na
Ushirika, Adam Malima.
Baadaye
baadhi ya wabunge nao walikoleza moto kwa kushinikiza mawaziri hao wang’oke,
huku wakiongeza idadi yao kwa kuwataja Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu
(Tamisemi), Hawa Ghasia na Manaibu wake, Aggrey Mwanri na Kassim Majaliwa
katika kundi hilo.
Mawaziri
hao waliitwa kujieleza mbele ya Kamati Kuu ya CCM kuhusu sababu za utendaji wao
kuwa wenye matatizo.
Hata
hivyo, kabla ya Rais Kikwete kuchukua hatua, alitengua uteuzi wa Mawaziri
wanne, Dk Emmanuel Nchimbi (Mambo ya Ndani), Shamsi Vuai Nahodha (Ulinzi na
Jeshi la Kujenga Taifa), Balozi Khamis Kagasheki (Maliasili na Utalii na Dk
Mathayo kutokana na mjadala mkali bungeni kuhusu jinsi Serikali ilivyotekeleza
Operesheni Tokomeza Ujangili.
Kadhalika,
Dk Mgimwa aliyefariki dunia Januari 5, mwaka huu alisababisha pengo la mawaziri
kufikia watano.
Wakati
Rais Kikwete alipofanya mabadiliko katika Baraza lake Januari 19, mwaka huu,
karibu mawaziri wote waliolalamikiwa walirejeshwa.
Hali hiyo ilizusha mjadala mkali kutoka kwa watu na makundi mbalimbali, huku CCM kupitia kwa Nape Nnauye kilisema kitaendelea kupiga kulele pale utendaji wa mawaziri hao utakapokuwa mbovu
>>Mwananchi
Hali hiyo ilizusha mjadala mkali kutoka kwa watu na makundi mbalimbali, huku CCM kupitia kwa Nape Nnauye kilisema kitaendelea kupiga kulele pale utendaji wa mawaziri hao utakapokuwa mbovu
>>Mwananchi

No comments:
Post a Comment