EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Sunday, January 19, 2014

UONGOZI WA MKOA MTWARA WAUNDA KAMATI SAIDIA NDADA ILI KUIKOMBOA TIMU

NA: KASSIM NGUMBI

UOngozi wa michezo mkoani mtwara ukiongozwa na afisa michezo wa mkoa ROGERS BAHATI wamekutana kuzungumzia namna ya kuisaidia timu ya ndanda na kuiwezesha kupanda daraja ili iweze kuifikisha katika kushiriki ligi kuu katika msimu wa mwaka 2014-2015.nadanda ndio timu pekee kwa sasa inayotegemewa na wakazi wa mkoa wa mtwara kuleta ligi kuu mkoan hapa mara baada ya kufeli kwa timu nyingine kongwe kama korosho na bandari hivyo katika kikao hicho kilichowakutanisha maofisa wa michezo wa mtwara vijijini Ndg:NIcolous Muya,afisa michezo manispaa Usura Kayombo na Afisa michezo wa mkoa pamoja na wadau wengine wa michezo mkoani hapa WAKIWEMO WAANDISHI WA HABARI NA kamati ya awali ya saidia ndanda ambapo maadhimio yaliyofikiwa ni kuishirikisha serikali moja kwa moja katika jambo hili kwa kumuhusisha mkuu wa mkoa wa mtwara Mh: Joseph Simbakalia na mkuu wa wilaya Mh: wilmani Kapenjama Ndile ili wao kama serikali waunde kamati mpya ya saidia ndanda itakayopewa nguvu na serikali ya mkoa.

lakini kwa upande wa wadau wameona ni vyema wakaandaa bonanza ambalo litashirikisha timu kongwe za CONGO na MITUMBA toka mtwara na mshindi wa bonanza hilo atakabidhiwa mbuzi huku mapato yote yakipelekwa kwa timu ya ndanda ambayo kwa sasa iko jijini dar es salaam ikijiandaa na michezo yake ya ligi daraja la kwanza na baadaye ije imalizie mechi nyingine huku nyumbani wakati huohuo timu hiyo ikiwa inaongoza katika kundi lake.hivi majuzi msemaji wa timu ya ndanda Kachele alisikika kwenye chombo kimoja cha habari cha hapa mtwara kupitia kipindi cha michezo alipokuwa akihojiwa tika dar es salaam kwa njia ya sim akikili timu hiyo kuchelewa kuingia kambini kutokana na ukata walionao huku timu zengine zikiwa tayari zimekwishaanza mazoezi mapema kwakuwa zina uwezo kifodha.

HAYA NI MAELEZO YA MAADHIMIO YA KIKAO CHA SAIDIA NDANDA SIKILIZA YAKIELEZWA NA KATIBU WA KAMATI HIYO YA SASA.........

No comments:

Post a Comment